Ndugu wananchi wa Mkoa
wa
Dar es
Salaam,
Tarehe 11/12/2012 siku
ya Jumanne kutakuwa na Sherehe za makabidhiano ya majengo ya huduma za mama na
mtoto katika Hospitali za Mnazi Mmoja, Sinza na Rangi tatu.Makabidhiano hayo
yatafanywa na Balozi wa Korea kusini kwa niaba ya watu wa Korea Kusini kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete.
Ndugu wananchi wa Mkoa
wa
Dar es
Salaam,
Makabidhiano hayo
yataanzia katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo katika Wilaya ya Ilala kuanzia
saa 2:30 asubuhi mpaka saa 5:00 asubuhi.Baada ya hapo makabidhiano hayo
yataelekea katika hospitali ya Sinza iliyopo katika Wilaya ya Kinondoni kuanzia
saa 5:00 asubuhi mpaka saa 7:00 mchana na kuishia katika hospitali ya Rangi Tatu
iliyopo katika Wilaya ya Temeke kuanzia saa 7:00 mchana mpaka saa 9:00
alasili.
Ndugu wananchi wa
Mkoa
wa Dar es
Salaam,
Wakati huo huo,Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete atazindua na kukabidhi
nyumba 36 za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto zilizojengwa katika eneo la
Msongola lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Makabidhiano hayo
yatafanyika kuanzia saa 8:00 mchana mpaka saa 10:00
jioni.
Ndugu wananchi wa
Mkoa
wa Dar es
Salaam,
Nawaomba mfike kwa wingi
kushuhudia makabidhiano ya majengo ya huduma za mama na mtoto katika Hospitali
za Mnazi Mmoja, Sinza na Rangi tatu pamoja na uzinduzi na kukabidhi nyumba 36 za
waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto.
Asanteni kwa
kunisikiliza.
Said Meck
Sadiki
MKUU WA MKOA
WA
DAR ES
SALAAM
10/12/2012
Post a Comment