Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu. Wanawake wengi wanalalamika kuwa hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao.Mara zote hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika, muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala. Wengi walioachana au kutalikiana nao walipitia njia hii pia.
Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu.
Njia za kukusaidia
1. kucheka pamoja
Kicheko
ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia
pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu,
kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya
katika vyote. Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu.
Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala
yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea. Kama utaanza kujizoeza hivi
ukiwa nyumbani, taratibu utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine
kokote.
2. Jifunzeni kutiana moyo
Kila
mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake. Jifunze kumtia moyo na
kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au
apendavyo. Onyesha heshima katika vitu hivyo pia. Kila upatapo nafasi
mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu. Mjenge mwenzako
mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee
yeye. Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo.
Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na
kutunyanyua na sisi pia.
3. Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu
ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote. Lazima
mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa
mmelala. Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au
mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na
njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili. Wengi wetu huweza
kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je,
ni aibu? au nidhamu mbaya? au dhambi?
Kugusana
ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri,
lini umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia
kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi
waliopweke wanaotamani kuguswa.
Mguso
huu wa upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema
kujifunza kuijenga lugha ya mguso wa tendo la ndoa katika mahusiano
yenu.
4. Zungumzeni hisia zenu
Kati
ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya
wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano. Lazima wapenzi wajifunze
kuzungumza kuhusu hisia zao. Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu,
mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu. Mpenzi wako hayuko kamili
na wala wewe pia sio mkamilifu. Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi
unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro
isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni
muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu. Mwambie
umpendae yapi yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza
kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa
maongezi ya simu utaongezeka.
5. Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe
tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu. Lazima tujifunze
kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia. Kutofautiana katika
mahusiano kuposana, na lazima tuwape
tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu. Kila hisia
za mmoja wetu zinaumuhimu. Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako
akuambie yanayo muumiza na msameheane.
6. Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara
nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko.
Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia
muonekano wetu lazima ume halisi na sio feki. Vile tunavyoviona katika
tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi. Kama tunataka tuonekane
sawa na vile tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na
kujizuia kuwa na mtazamo bora katika mahusiano yetu. Ukianza kupata
ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji
ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu
mlionao.
Lengo
liwe kuvitafuta vile vyote mpenzi wako alivyonavyo ambavyo hukuza
ukaribu wenu. Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha
yako.
KWA HISANI YA samsasali.blogspot.com/
Post a Comment