Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi, (kushoto) akifurahia
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Huru Tanzania (EPZA) Dkt.
Adelhelm Meru muda mfupi mara baada ya kukutana na ujumbe wa wawekezaji kutoka
nchini china mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Raymond Mbilinyi, (kushoto) akifurahia
jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Huru Tanzania (EPZA) Dkt.
Adelhelm Meru muda mfupi mara baada ya kukutana na ujumbe wa wawekezaji kutoka
nchini china mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
Juhudi za serikali
kutangaza vivutio vyake vya uwekezaji zinazidi kuzaa matunda baada ya ujio wa
ujumbe wa watu sita wa kampuni ya Anhui Foreign Economic Construction ya nchini
China kuja nchini kujionea na kujua fursa mbalimbali wanazoweza kuwekeza hapa
nchini.
Akiongea na waandishi wa
habari kuhusiana na ujio huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi alisema ujumbe huo ni wa wawekezaji wakubwa
kutoka China wanaotaka kuwekeza hapa nchini kwa ushirikiano na serikali ya
Tanzania.
“Hii ni fursa nyingine
ambayo nchi inapata kupitia uwekezaji, hawa ni wawekezaji wakubwa ambao wamekuja
kwa lengo la kuangalia fursa mbalimbali hapa nchini,” alisema Bw. Mbilinyi
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa ujumbe
huounaoongozwa na mwenyekiti wake wa bodi, Bw. Jiang Qingde umeshaonana na Rais
Jakaya Kikwete na kuzungumza naye mambo mbalimbali juu ya ujio wao hapa
nchini.
“Ni kampuni yenye uzoefu wa
hali ya juu katika sula la uwekezaji,” alisema.
Akielezea zaidi alisema
mpaka sasa wamewekeza katika nchi zipatazo 20 katika bara la Afrika hivyo kuja
kwao hapa nchini ni ishara kuwa Tanzania pia ina mazingira mazuri ya uwekezaji
na kwamba jitihada za TIC kutangaza fursa za uwekezaji hapa nchini zinazaa
matunda.
Alisema kuwa wawekezaji hao
wana uzoefu mkubwa katika sekta za madini, viwanja vya ndege, na nishati ya
umeme.
Alisema kwa upande wa
viwanja vya ndege tayari kampuni hiyo imeweza kuwekeza katika katika nchi 15
katika bara la Afrika, na kuongeza kuwa wana uzoefu wa kutosha katika suala la
uwekezaji katika maeneo mengi ya Afrika.
Alisema kuwa uzoefu
walionao wawekezaji hao utasaidia sana katika sula la kukuza uchumi wa nchi na
kuongeza ajira hapa nchini kwa kuwa uwekezaji wao ni wa maeneo mengi kwa wakati
mmoja hivyo ni fursa ya kipekee kwa nchi katika kutengeneza ajira kupitia sekta
ya uwekezaji toka nje.
“Kuna tatizo la ajira kwa
vijana wetu, hivyo kuwepo kwa fursa za uwekezaji hapa nchini ni jambo jema kwa
serikali yetu kuondokana na tatizo hili kwa kiasi kikubwa,” alisema Bw. Mbilinyi
na kuongeza kuwa TIC itaendelea na juhudi zake za kutangaza vivutio vya
uwekezaji Tanzania kwa wawekezaji wa ndani na nje.
Tanzania ina mahusiano
mazuri ya kijamii na kiuchumi na watu na serikali ya China.
Kampuni mbalimbali toka
nchi hiyo ambayo inapiga hatua kubwa kiuchumi kwa kasi zimekua zikifanya kazi
hapa Tanzania kwa miaka kadhaa hasa katika sekta ya ujenzi wa vitu
mbalimbali.
Post a Comment