Kikosi cha zamani cha Taifa Stars
Kikosi cha Kilimanjaro Stars kilichoriki Tusker Challenge Cup Uganda
Kikosi cha Zanzibar Heroes kilicho shika nafasi ya 3 Tusker Challenge Cup Uganda.
WAKATI vikosi vya timu za Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes vilivyokuwa vinashiriki michuano ya Kombe la Tusker Cecafa Chalenji jijini Kampala, vinarejea Dar es Salaam na Zanzibar hii leo, kesho Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania anataraji kutanga kiksi kipya cha timu hiyo.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen kesho Jumatatu saa sita mchana katika Ofisi za Shirikisho la Soka nchini anataraji kutangaza kikosi hicho ambacho dhahiri kitaundwa na Wachezaji wa timu mbili za taifa za Bara na Visiwani ambazo zilishiriki michuano iliyomalizika jana jijini Uganda na kuonesha uwezo wao mkubwa kisoka.
Kikosi chake hicho kipya kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12, 2012 jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22, 2012 katika Uwanja wa Taifa.
Jumapili (Desemba 9, 2012). Timu hiyo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 11 kamili jioni kwa ndege ya Precision Air.
Post a Comment