IMEELEZWA kwamba ujasiriamali na kilimo ni sekta zitakazoikomboa Tanzania
kutoka kwenye janga la ukosefu wa ajira, tofauti na nchi tajiri zinazotegemea
viwanda na kampuni kubwa za biashara na huduma katika kutengeneza ajira kwa watu
wao.
Hayo yalibainishwa juzi na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, alipofungua semina ya siku moja ya wajasiriamali wanawake wapatao 300 wa Kata ya Kipawa, Segerea, wilayani Ilala.
Dk. Mahanga ambaye ni Mbunge wa Segerea, alisema kuwa kutokana na Tanzania kutokuwa na viwanda vingi na vikubwa, pia sekta ya umma na makampuni binafsi kuwa na uwezo mdogo wa kuajiri, taifa litaendelea kutegemea kilimo, ufugaji, uvuvi na ujasiriamali katika kukabiliana na ukosefu wa ajira.
Alisema kuwa asilimia tano kati ya vijana 800,000 wanaoingia kwenye soko la ajira kila mwaka, ndio wanaoajiriwa kwenye sekta rasmi ya umma na kampuni binafsi.
Mahanga alisema sababu kubwa ya wajasiriamali wengi kushindwa katika biashara zao ni kukosa ustadi katika shughuli zao, kutojua kutenganisha biashara zao na mambo binafsi, kutoweka kumbukumbu na hesabu za biashara, kushindwa kulinda mitaji yao na kurudisha mikopo ya biashara.
Chanzo: Tanzania Daima

Post a Comment