Mahmoud Ahmad Arusha
Viongozi wa madhehebu mbali
mbali ya dini wametakiwa kudumisha umoja na mshikamano sanjari na kuacha
kudharaulina kwani hilo litaleta kumong’onyoka kwa maadili na kubomoa amani yetu
na badala yake kuhubiri ushirikiano na kuwajenga waumini wao kuwa na hofu ya
mungu.
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu mkuu wa CCM ndugu Abdurahaman Kinana kwenye
maadhimisho ya siku ya kumbu kumbuya Imamu Husein yanayoadhimishwa na dhehebu
la Khoja Ithnasher kote duniani na kufanyika kwenye msikiti wa jamii hiyo jijini
hapa juzi.
Kinana alisema kuwa hivi
sasa jamii ya watanzania imeingia kwa baadhi ya watanzania kuwauza wenzao huku
ni kutaka kuleta mpasuko kiimani na wengine kujenga uadui kwa kudharau madhehebu
za wenzao tufike mahali tuheshimu na kujifunza yale yalio kwa mwenzako kwa
ustaarabu na kuvumiliana.
“Ustaarabu wa kuvumiliana
na kuweka upendo miongoni mwetu ndiyo silaha ya kuitunza amani iliyopo hapa
nchini nawaombeni viongozi wa dini hapa nchini kuwajenga waumini kuwa na hofu ya
Mungu ili taifa letu lisikumbwe na mipasuko ya kiimani”alisema
Kinana
Akizungumza kwa niaba ya
mkuu wa mkoa huo Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga alisema kuwa kumekuwa
na vikundi vya kiimani ambavyo vimesajiliwa lakini vimekuwa vikichochea uvunjifu
wa amani na kuvitaka kuacha kuipoteza amani iliyopo kwani kutafuta ni gharama
kuliko kuitunza
Kasunga alisema kuwa anatoa
wito kwa viongozi wa madhebu hapa nchini kuwajengea hofu ya Mungu watumishi wa
serikali na wananchi ilituishi salama kwa amani , serekali pekee haiwezi
kuitunza bila ya kushirikiana nanyi na watanzania wote.
Nae Sheikh wa mkoa wa
Arusha Shaban Bin Simba alisema kuwa nchi kuingia kwenye machafuko ni jamii
kumuasi muumba wao na kutokuwa na hofu ya siku ya malipo na kuwataka viongozi wa
dini kujenga ushirikiano wa karibu na masikilizano
Post a Comment