Mwanamuziki Kofii Olomide akiimba
jukwaani na kundi lake katika Onesho linalofanyiki usiku huu kwenye viwanja
vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam ambapo wageni waalikwa na mashabiki
mbalimbali wamefurika katika viwanja hivvyo , ili waweze kushuhudia shughuli
pevu ya mwanamuziki huyo nguli wa muziki Barani Afrika.
Fullshangweblog na kikozi kazi chake chote iko
katika eneo la tukio ili kukumuvuzishia matukio yatakayojiri katika viwanja vya
Leaders usiku huu moja kwa moja katika kukupasha habari na kukuburudisha
pia.
Mmoja wa wanenguaji wa mwanamuziki Kofii
Olomide akifanya vitu vyake jukwaani kama anavyoonekana katika
picha.
Kofii Olomide akiimba na mmoja wa waimbaji wake Cindy.
Mwanamuziki Kofii Olomide akiwa na mmoja wa waimbaji wake
wa kike wakipagawisha mashabiki wa bendi hiyo waliojitokeza kwa wingi katika
viwanja vya Leaders ili kushuhudia kile anachokifanya
jukwaani.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Clouds Media Group akizungumza
kumshukuru mwanamuziki Kofii Olomide na mashabiki waliojitokeza kwa wingi katika
onesho hilo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es
salaam.
Vimwana wanenguaji wa
mwanamuziki Kofii Olomide wakimwaga mauno kwa kwenda mbele jukwaani katika
onesho hilo.
Mwanamuziki Kofii Olomide akiwa
amezungukwa na vimwana hao ambao ni wanenguajia wa bendi yake huku akiwa
katikati yao kama mfalme.
Hapa ni Burudani ya mauno tu kama inavyoonekana
madau.
Mashabiki mbalimbali wa
mwanamuziki Kofii Olomide wakifuatilia kwa makini wakati mwanamuziki Kofii
Olomide akiimba jukwaani.
Mashabiki wa mwanamziki Kofii
Olomide wakishangilia kwa furaha wakati mwanamuziki Kofii Olomide akiimba
jukwaani.
Mwanamuziki Kofii Olomide akiwa
katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Steve
Gannon wa pili kutoka kushoto na Mkurugenzi wa Masoko Bw. Ephraim Mafuru pamoja
na wafanyakazi wengine
KWA PICHA ZAIDI YA MAMBO YALIVYOKUWA KWENYE SHOW HIYO BOFYA "Read More" hapo chini
Wanamuziki wa bendi ya African Stars wakifanya vitu vyao katika
Jukwaa la Tusker Canival kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es
salaam likiwa ni onesho la Utangulizi kabla ya mwanamuziki nguli wa muziki wa
kiafrika Kofii Olomide ambaye anatarajiwa kupanda jukwaani muda mfupi ujao ili
kuwapa burudani mashabiki wake ambao wamefurika katika viwanja hivi , ili waweze
kushuhudia shughuli pevu ya mwanamuziki huyo jukwaani.
Twanga Pepeta ni
raha tupu katika jukwaa la Tusker Carnival kama wanavyoonekana hapo jukwaani
wakiwajibika vilivyo.
Hachezi mpira wa miguu ila yuko katika
kuburudisha mashabiki wake yote ikiwa ni burudani.
Mboni Masimba wa kipindi cha Mboni Show
kinachorushwa na EATV akiwa na wageni wengine waalikwa katika jukwaa maalum
katika onesho la Mwanamuziki Kofii Olomide linalofanyika usiku huu kwenye
viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam
Kutoka kushoto ni Azda Amani
kutoka SBL, Caroline Owenya na Antonina Kongoro wakipozi kwa
picha.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Bw. Steve
Gannon, Anitha Msangi Maurice Njowoka, Agness Kiondo, Ada Amani na Nandi
Mwiyombela wakipozi kwa picha.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotion Juhayna Kusaga kulia
akiwa katika picha ya pamoja na marafiki zake katika onesho
hilo.
Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti wakijimwaga kwa
kuserebuka na muziki uliokuwa ukitumbuizwa na mwanamuziki Kofii
Olomide.
Wafanyakazi wa kampuni ya ndege ya Fastjet wakiwa
katika onesho hilo , kutoka kushoto ni Geraldine Duwe Mkuu wa Utawala ,Prisca
Simon Kitengo cha Mahusiano kwa wateja na Gladness Nahutwa Mkuu wa Mkuu wa
masoko Mtandaoni.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim
Mafuru wa pili kutoka kushoto na Mdau Teddy Mapunda watatu kutoka kushoto
wakipozi kwa picha na wafanyakazi wa kampuni ya bia ya
Serengeti.
Wanamuziki wa bendi ya Diamond Misica wakifanya vitu vyao
jukwaani kama wanavyoonekana.
Kutoka kulia ni Azda Amani, Agness Kiondo, Maurice Njowoka,
mdau Teddy Mapunda na Caroline Owenya wakipozi kwa picha ya
pamoja.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim
Mafuru akiwa katika picha ya pamoja na mdau Teddy Mapunda katika onesho
hilo.
Kutoka kulia ni Agness Kiondo, Caroline Owenya,Azada Amani
na Antonina Kongoro wakipozi kwa picha
.
Mmoja wa wanenguaji mahiri wa bendi
ya Mapacha Watatu Salma Mjukuu akifanya vitu vyake jukwaani wakati bendi hiyo
ilipokuwa iifanya onesho la utangulizi kabla ya mwanamuziki Kofii Olomide
kupanda jukwaani kwenye viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam usiku huu
ambapo mashabiki wanamziki kumiminika katika viwanja hivyo ili kushumshuhudia
Gwiji huyo wa muziki Afrika.
Wanenguaji wa bendi ya Mapacha
watatu wakio0nyesha uwezo wao katika jukwaa moja na mwanauziki Kofii Olomide hii
ni nafasi nzuri kwa bendi hiyo kuonyesha kiwango chake katika muziki wa Tanzania
katikati ni Jose Mara mmoja wa viongozi wa bendi hiyo
Hapa ni burudani kwa kwenda
mbele kutoka Mapacha Watatu.
Kaazi
kwelikweli.
on Sunday, December 16, 2012
Post a Comment