Kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na mashirika mengine, yamefanikiwa kufanya
maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani, miaka 64 ya Tamko la Kimataifa
la Haki za Binadamu, la mwaka 1948 na Kilele cha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa
Jinsia.
Mambo mbalimbali
yalifanyika, ikiwa ni pamoja na maandamano, mawasilisho ya hotuba mbalimbali na
burudani kutoka kwa vikundi mbalimbali vikiwemo Jakaya Arts Theatre, Dancers wa
Kibasila Secondary, Maigizo Human Rights Clubs kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu
(UDSM, IFM, Tumaini, Mwl. Nyerere) na kasha mjadala wa pamoja, uliojikita zaidi
kwenye uadilifu na hatma ya taifa letu.
Mgeni rasmi katika siku
hii alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa LHRC, Askofu Mstaafu Elinaza E.
Sendoro (aliyewakilishwa na Wakili Fransic Stolla - Rais wa Chama cha Wanasheria
wa Tanganyika), wawakilishi wa Umoja wa Ulaya, Mkurugenzi Mtendaji wa WiLDAF
mama Judith Odunga, Mkurugenzi Mtendaji wa WLAC, na wawakilishi kutoka mashirika
mbalimbali na wanaharakati toka pande mbalimbali za Dar es Salaam.
Post a Comment