Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha
Bilal, wakimsalimia Mzee Said Noor Abdulkadir, wakati alipomtembelea kumjulia
hali nyumbani kwake, Tunduni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, jana Desemba
23, 2012. Mzee huyo anasumbuliwa na maradhi ya mguu kwa muda wa miaka
13.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Viongozi
wa Kituo cha Mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka na wananchi wa kijiji hicho, wakati
alipofika katika kituo hicho leo Desemba 24, 2012 kwa ajili ya kujionea
maendeleo ya kituo hicho, akiwa ameongozana na mkewe Mama Asha
Bilal.
Sehemu ya Kompyuta
zilizopo katika Kituo hicho cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mjumbe
wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Chwaka, Hamis Himid Ramadhan, wakati
alipotembelea kukagua maendeleo ya Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka
(CCTC) leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea ramani ya ujenzi
mpya wa shule ya Chwaka, kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Fadhili Hamada
Mshamba, wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Kituo cha mafunzo ya Kompyuta
cha Chwaka (CCTC) leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha
Bilal, wakiondoka katika Kituo cha mafunzo ya Kompyuta cha Chwaka (CCTC) baada
ya kutembelea na kukagua maendeleo ya kituo hicho leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal,
wakizungumza na Mzee Silima Jendele, wakati Makamu alipokuwa katika ziara yake
ya kutembelea Wazee leo, katika Mkoa wa Kusini Unguja.
Post a Comment