MAMA
wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ametoa baraka zake kwa mwigizaji
chipukizi, Philemon Lutwaza ‘Uncle D’ ambaye anatarajia kuigiza katika filamu ya
After Death ambayo ni maalum kwa kumuenzi marehemu mwanaye, Imelda Mtema
anashuka nayo.
Akizungumza na paparazi wetu juzikati, mama Kanumba
ameweka plain kuwa ameridhishwa na uwezo wa Uncle D na anaimani kuwa ataweza
kuziba pengo la marehemu katika nafasi ya kucheza na watoto wale aliokuwa
akiigiza nao marehemu
Namshukuru sana Jacqueline Wolper kwa kuandaa filamu
ya After Death maalum kwa ajili ya kumuenzi mwanangu. Nina imani kila kitu
kitakwenda vizuri na mimi nimewapa baraka zote ,” alisema mama
huyo.
chanzo:globalpublishers



Post a Comment