Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kuwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Nelson Mandela atasalia hospitalini msimu huu wa Krismasi.
Bwana Mandela ambaye ni rais mweusi wa kwanza nchini Afrika Kusini, alilazwa hospitali wiki mbili zilizopita kufuatia maambukizi ya mapafu na uvimbe au mawe kwenye kibofu.
Kuna wasi wasi mkubwa nchini Afrika kuhusu afya yab rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 94.
Mandela alifungwa miaka 27 baada ya kupatikana na hatia ya kuongoza uasi dhidi ya serikali ya Wazungu walio wachache nchini humo.
Raia wengi wa nchi hiyo wanamuona kama baba wa taifa kutokana na juhudi zake ya kupigania uhuru wa taifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali, Bwana Mandela atasherehekea siku kuu ya Krismasi akiwa hospitalini.
Mwandishi wa BBC, mjini Johannesburg, anasema kila kukicha kuna hali ya wasi wasi kuhusu afya ya rais huyo wa zamani.
Awali kulikuwa na matumaini kuwa Bwana Mandela huenda akaruhusiwa kwenda nyumbani, lakini madaktari wake wanasema hawako tayari kumruhusu Bwana Mandela kwenda nyumbani.
Licha ya rais Zuma kutangaza kuwa Afya ya rais huyo wa zamani sio nzuri sana, Rais Zuma amesema anaendelea kupata nafuu.
Serikali ya Afrika Kusini imesema Mandela anatibiwa kufuatia maambukizi ya Mapafu katika hospitali moja mjini Pretoria.
BBC/SWAHILI
Post a Comment