|
Messi akiumia kwa kugonga goti kwenye kwapa la
kipa wa Benfica, Artur Moraes wakati wa mechi yao ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
Jumatano ambayo ilimalizika kwa sare ya 0-0. |
|
Mbishi... Licha ya kuumia Messi
bado alimpita kipa na kujaribu kufunga lakini kipa alirudi haraka na
kudaka mpira huo. |
|
Kisha akakaa chini kusikilizia
maumivu |
|
Akajaribu
kuinuka.... |
|
Lakini wapi bhana, akarudi
chini.... |
|
Kisha akalala chini
kabisa.... |
|
Mbio mbio madaktari
wakawahi... |
|
Wasiwasi wako tu kijana. Mi sioni kama una tatizo
kubwa hapa |
|
Hebu panda kwenye hiki kigari tukakupime
freshi... |
|
Usijali jembe... rekodi ya Gerd Muller utaifikia
tu... kwani si umebakisha goli moja tu? |
NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi amesema anajisikia
yuko poa kabisa baada ya kuhofiwa kuumia goti katika mechi yao ya Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya dhidi ya Benfica Jumatano.
Messi alitolewa kwa machela baada
ya kugongana na kipa wa Benfica, Artur Moraes, lakini presha zilishuka baada ya
uthibitisho kutolewa muda mfupi baadaye kwamba maumivu hayakuwa mabaya zaidi ya
mchubuko tu kwenye goli lake la kulia.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa
Argentina alikuwa akijifua kwenye gym wakati wachezaji wenzake wakifanya mazoezi
uwanjani jana, na Messi alisema bado ipo nafasi ya yeye kucheza mechi yao ya
Jumapili.
"Najisikia vyema, lakini sijui kama nitakuwa tayari kucheza
mechi ya Jumapili," alisema katika tukio la promosheni kwenye Uwanja wa Nou Camp
jana. "Nitaona. Nina faraja kwa meseji zote na sapoti niliyopata."
Messi
alisema aliumia wakati alipogongana na Moraes, lakini alijaribu kufunga kwa
shuti la mkunjo wa ndizi kabla ya kuanguka "sakafuni" huku akiwa ameshikilia
goti lake.
"Nilidhani kwamba lingekuwa shuti langu la mwisho hadi baada
ya muda mrefu sana," alisema. "Hivyo nikaamua kucheza kamari kwa kupiga mpira
langoni."
Aliongeza: "Ukweli ni kwamba sikufikiria chochote kwa sababu
nilichokuwa nacho pale ni maumivu tu. Lakini kwa wakati ule nilidhani ni
majeraha mabaya. Nilipoambiwa kwamba si makubwa nikatulia."
on Friday, December 7, 2012
Post a Comment