BAADA ya Waziri
wa
Ofisi ya
Makamu wa Rais (Mazingira), kuwashukia viongozi wa jiji kuwa ndiyo chanzo cha
kukithiri uchafu jijini, Meya wa jiji hilo Dk Didas Masaburi amejibu kwa kusema
tuhuma hizo hziwahusu.
Kauli hiyo ilitolewa jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, na Meya huyo wakati alipokuwa akizungumza na
wandishi wa habari kuhusu kikao cha kufunga mwaka 2012.
Masaburi alisema kauli ya
waziri huyo, inaonekana kujichanganya kwani kazi ya kuliweka jiji hilo katika
hali ya usafi siyo ya jiji bali wahusika wakuu ni
Halmashauri.
Alisema kazi kubwa ya mamlaka
ya jiji ni kusimamamia hali ya usafi usafi wa dampo liliko Pugu
Kinyamwezi.
“Hizo lawama wanapaswa
wazielekeze kwenye Halmashauri kutokana na wenyewe kushindwa kupeleka taka na
siyo sisi jiji, kama wenyewe hawatuletei taka dampo na
alaumiwe”alisema.
Dk
Masaburi anastajabishwa, utaratibu unaotumiwa na baadhi ya mawaziri kwa
kuzishambulia Halmashauri kuwa zinafuga uozo wa uchafuzi wa mazingira, ambapo
hata huko kwenye ofisi za wizara zao upo uchafu.
Alitoa wito kwa Serikalli Kuu
kubadili utaratibu wake kwa kuzitengea fedha za kutosha Halmashauri hizo na
kuzifikisha kwa wakati, lengo likiwa ni kwenda sambamba na sheria ya mazingira
ya mwaka 2004.
Alisema vyanzo ya mapato
wakati mwingine vinaweza kuwa chanzo cha Halmashuri hizo kushindwa kusimamia
sheria hiyo ya utunzaji wa mazingira.
Post a Comment