Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia waumini wa Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania usharika wa Msasani jijini Dar es Salaam
wakati wa sherehe za uzinduzi wa DVD ya Kwaya na harambee ya ununuzi wa basi la
kwaya ya Kanisa hilo,iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Mh. Lowassa ambaye
aliongozana na familia yake yote, alichangia shilingi millioni 10, huku wanawe
wakitoa kiasi cha shilingi milioni tano.
Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akipongezwa na Mchungaji
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania usharika wa Msasani,Eliguard Muro
mara baada ya kuhutubia na kuzingua DVD ya kwaya ya Kanisa hilo na kuendesha
Harambee ya Kuchanfia Ununuzi wa Basi la Kwaya ya Kanisa hilo,iliyofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya
CRDB,Dk. Charles Kimei (kulia) akiwahamasisha waumini wengine kujitokeza
kuchangia Harambee hiyo,ambapo yeye binafsi aliweza kuchangia kiasi cha Sh.
Milioni 7 katika harambee hiyo.Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo
la Monduli,Mh. Edward Lowassa ambaye ndie alieiongoza harambee
hiyo.
Mdau Richard Kasesela
akichangia kiasi cha Dola 300 katika harambee hiyo
Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na Mkewe Mama
Regina Lowassa kabla ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa DVD ya Kwaya na
harambee ya ununuzi wa basi la kwaya ya Kanisa hilo,iliyofanyika leo jijini Dar
es Salaam.
Mke Waziri Mkuu
Mstaafu,Mkewe Mama Regina Lowassa (kushoto) akiwa na Familia yake wakati
wa sherehe za uzinduzi wa DVD ya Kwaya na harambee ya ununuzi wa basi la kwaya
ya Kanisa hilo,iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
Post a Comment