Na
Abdulaziz,Lindi
UPEPO mkali uliombatana na
mvua kubwa umeziathiri baadhi ya nyumba huku shule ya sekondari ya Mnacho
wilayani Ruangwa ikipata athari kwa kiasi kikubwa baada ya madarasa sita
kuezuliwa mabati na baadhi ya wanakijiji kupata majeraha na kusababisha wakazi
wengine kukosa mahali pa kuishi.
Upepo huo uliotokea jana ni
mfufulizo wa matukio hayo kwa vijiji vya kata hiyo ambapo awali mwanzoni mwa
mwaka huu uliezua madarasa mawili ya shule hiyo.
Akitoa taarifa ya maafa hayo
ya jana katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Ruangwa leo,
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo,Bw Reubern Mfune alieleza kuwa
Kufuatia kuwepo kwa tukio hilo lilitokea jana jioni Ofisi yake ilifika eneo la
tukio akiwemo na mkuu wa wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzira na tayari
wamepelekwa wataalamu kutathimini athari hizo ili shule hiyo inayotarajiwa
kuanza muhula jan 14 Halmashauri yake itashirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya
kuhakikisha hali ya shule inakamilishwa.
Aidha Mkurugenzi alibainisha
katika kikao hicho cha baraza la madiwani kuwa Katika maafa hayo ambayo kwa
kiasi kikubwa yaliathiri shule hiyo bado ni changamoto katika Halmashauri yake
kufuatia kupangawa kupokea wanafunzi 92 wa kidato cha kwanza na inatarajiwa
kufunguliwa jan 14,2013 Katika maafa hayo Mtu mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa
hospitalini
Post a Comment