Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MWAKA 2012 ULIKUWA NI MWAKA WA UCHAGUZI KWA CHAMA CHA MAPINDUZI. YAFUATAYO NI BAADHI YA MATOKEO NGAZI ZA TAIFA

Rais Jakaya Kikwete amechaguliwa na kushinda kwa kishindo uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM taifa kwa kupata kura 2395.kati ya 2397 zilizopigwa hii leo. Kwa matokeo hayo Ndugu Jakaya Kikwete ameitetea vyema nafasi yake hiyo hadi mwaka 2017. Huku kura za hapana zikiwa 2. Sawa na asilimia 99.92.



Aidha wagombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambazo kwa upande wa Bara ilikuwa ikigombewa na Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Philip Mangula na amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kwa kura 2397, huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar ameshinda Raius wa Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein kwa kupata kura zote zilizopigwa 2397. Ushindi wa Shein na Mangula kushinda kwa kura za Ndio kwa Asilimia 100.



Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete



Makamu Mwenyekiti- Bara wa CCM, Philip Mangula



Makamu Mwenyekiti - visiwani Dkt. Shein

RAIS KIKWETE ATANGAZA KIKOSI SUPER CHA SEKRETARIETI MPYA YA CCM



Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM, Taifa
Mwigulu Nchemba-Naibu Katibu Mkuu (Bara)
Vuai Ali Vuai-Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
Nape Nnauye-Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
Asha-Rose Migiro- Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Zakia Meghji-Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha
Muhamed Seif Khatib, Katibu wa NEC, Oganaizesheni:Picha zote na Bashir Nkoromo)
*******************
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kimekutana katika Ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya chama, maarufu kama Whitehouse mjini Dodoma,leo tarehe 14th Nov 2012.

Kikao hicho kitajadili juu ya kuunda na kupitisha majina yaliyopendekezwa na Mwenyekiti wa ChaCha Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama ya Taifa (CC) pamoja na uundaji wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa. Ambapo Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, anayo fursa ya kuteua wajumbe kumi(10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita (6) miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape nnauye na Mhe. Abdulrahaman Kinana .
Baada ya uteuzi huo Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina yafuatayo;

  1. Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman kinana.
  2. Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mhe. Vuai Ali Vuai.
  3. Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Madelu Nchemba.
  4. Katibu wa Oganaizesheni ni Ndugu Mohamed Seif Khatibu.
  5. Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.
  6. Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji.

MATOKEO YA UNEC CCM NGAZI YA TAIFA, HAYA HAPA



Matokeo ya chaguzi za nafasi 10 za wajumbe wa NEC Tanzania Bara wa Chama cha Mapinduzi zinazoendela Dodoma yametoka ni kama ifuatavyo:


1. Stephen Wassira - 2,135
2. January Makamba – 2,093
3. Mwigulu Nchemba – 1,967
4. Martine Shigela – 1,824
5. William Lukuvi – 1,805
6. Bernard Membe – 1,455
7. Mathayo David Mathayo – 1,414
8. Jackson Msome - 1,207
9. Wilson Mukama - 1,174
10. Fenela Mukangara - 984



Matokeo rasmi ya UNEC Viti 10 Visiwani, walioshinda ni:

1. Hadija H. Abood
2. Shamsi Vuai Nahodha
3. Dkt. hussein Mwinyi
4. Abduliham Cosmas
5. Mohammed Seif Khatibu
6. Bhagwaji M. Mshamba (Banyiani)
7. Makame Mbalawa
8. Omary Yusuph Mzee
9. Hamis Mbeto Mamo
10. Dkt. Abdalla Juma SADALLA








WENYEVITI WA JUMUIYA:
 
1. JUMUIYA YA WAZAZI - ABDALLAH BULEMBO
2. JUMUIYA YA WANAWAKE - SOPHIA SIMBA
3. JUMUIYA YA VIJANA - KHAMIS SADIFA JUMA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top