MIONGONI mwa mambo yatakayokumbukwa katika kesi iliyotengua na baadaye kumrejeshea ubunge, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ni mawakili wa pande mbili zilizokuwa zikipambana katika kesi hiyo ya kuhistoria.
Kwanza ni mawakili ndugu; Tundu Lissu ambaye alikuwa akimtetea Lema na Alute Mughway ambaye alikuwa wakili wa makada wa CCM waliofungua kesi kupinga ushindi wa Lema.
Lissu ambaye ni kada wa Chadema na Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakili mwenzake, Method Kimomogolo walishirikiana kumtetea Lema ambaye ni kada wa Chadema.
Lakini kaka yake (Mughway) alikuwa anawatetea warufaniwa (wajibu rufaa) ambao ni makada wa CCM; Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel.
Alute na Tundu wote ni watoto wa Mzee Augustino Lissu Mughwai na Bibi Alu Alute Tundu ambao wote sasa marehemu. Wakati Alute ni mzaliwa wa pili katika familia hiyo ya watoto 12, Tundu ni mzaliwa wa tano.
Alute hivi sasa ni wakili wa kujitegemea akifanyika kazi zake mkoani Arusha wakati mdogo wake Tundu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki ni wakili akifanyia kazi zake jijini Dar es Salaam.
Ndugu hawa walikuwa kivutio katika kesi hiyo kwani wote walionekana kuwa mahiri katika kujenga na kupangua hoja pale walipokuwa wakiishawishi mahakama kuwapa ushindi wateja wao.
Ndugu hawa wawili wamekuwa wakipambana mahakamani kwenye kesi ya Lema tangu ifunguliwe Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, wakipinga matokeo yaliyompa ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Hukumu ya kesi hiyo ndiyo iliyomvua ubunge Aprili 5, 2012 lakini Lissu na wakili mwenzake Method Kimomogolo awalikata rufaa ambayo jana ilimrejeshea Lema Ubunge.
Hii inatoa picha kwamba katika fani ya ya sheria hasa kwenye uwakili mahakamani huweza kuwakutanisha maadui kutoka pande mbili, mtu na mwanaye katika pande hizo mbili lakini kila mmoja akisimamia kile anachokiamini ili kufanya kazi yake.
Baba anaweza kuwa upande wa utetezi na mtoto anaweza kuwa upande wa mashtaka, kila mmoja akitaka kuonyesha uwezo wake kwa mteja wake.
Wakati mwingine watu huweza kusema kwa nini huyu asizungumze na mwanaye ili asitoe hoja nzito au mtoto asizungumze na baba yake ili asitoe hoja nzito ili kurahisisha kesi. Lakini hayo hayana nafasi pale watu hawa wanapokuwa katika kazi zao hasa za kitaaluma.
Chanzo: Mwananchi
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
Hatuna huruma, tunabeba vyote-Dk. Biteko9 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment