NAPENDA
kutoa taarifa kwa umma kutokana na habari zinazoandikwa kwenye baadhi ya vyombo
vya habari, huku chanzo cha habari hizo kikiwa ni Katibu wa BAVICHA Mkoa wa
Tanga, Bwana Deogratias Kisandu, ambazo zimekuwa zikionesha kuwa vijana wa Mkoa
wa Tanga tuna walakini katika chama chetu cha CHADEMA.
Leo
katika baadhi ya vyombo vya habari, Bwana Kisandu amenukuliwa akitoa taarifa
kuwa yeye pamoja na makatibu wenzake nchi nzima, wamepanga kufanya maandamano
ya kuupinga uongozi wa juu wa kitaifa wa BAVICHA.
Kwa
kutambua na kuheshimu kuwa moja ya misingi muhimu ya uendeshaji wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na mabaraza yake ni vikao, ambavyo
vipo kwa mujibu wa Katiba, miongozo, taratibu, kanuni na itifaki za chama,
vijana wa CHADEMA Mkoa wa Tanga, ambao mimi ndiye msemaji wao kikatiba,
tunaamini Bwana Kisandu anazidi kupotoka.
Kwa hiyo
basi, kama ambavyo nimeshapokea malalamiko kutoka kwa vijana wa Tanga baada ya
hatua yake ya awali ya Bwana Kisandu kutoa taarifa kwa vyombo vya habari, bila
kuzingatia katiba, maadili na itifaki ya chama, akibeba propaganda nyepesi za
Sekretarieti ya CCM, juu ya suala la kadi mbili kwa Katibu Mkuu wetu Dkt.
Willibrod Slaa, kuna haja ya kufanya vikao kuangalia na kujadili mwenendo wa
kiongozi mwenzetu huyo.
Kwa
sababu kama vijana makini wa CHADEMA, chama ambacho kinaamini katika kutoa
utumishi bora, mikakati madhubuti, sera imara kwa ajili ya maendeleo endelevu
ya Watanzania wote, ambao wamekosa uongozi bora na siasa safi kutokana na
ufisadi na ubadhirifu wa CCM, lazima tuwe makini na kila mwenzetu yeyote yule
ambaye anaonekana kufanya kazi ya CCM kwa kutumia jina la
CHADEMA.
Tunapenda
kumkumbusha Bwana Kisandu kuwa atumie muda wake pia kuisoma vyema
katiba ya
CHADEMA hasa katika Sura ya 10 inayozungumzia Maadili ya Viongozi, Sifa
mahususi za viongozi na maadili ya wanachama, kifungu
10.1(1-13), toleo
la mwaka 2006.
Kuhusu
masuala ya ushiriki wa vijana kwenye shughuli mbalimbali za chama ikiwemo
mikutano ya M4C, Bwana Kisandu anapaswa kuelewa kuwa vijana kutokana maeneo
mbalimbali ya nchi, ukiwemo Mkoa wa Tanga tumekuwa tukishirikishwa, kupitia
utaratibu maalum unaopangwa na Ofisi ya Katibu Mkuu, ambao tunaamini mpaka sasa
umetoa fursa kwa wanachama wote, wakiwemo wazee, wanawake na vijana kukieneza
na kukiimarisha chama maeneo mbalimbali ya nchi.
Na
maamuzi yote ya msingi kwa uendeshaji wa Baraza hasa kwa Mkoa wa Tanga
yatafanyika kupitia vikao na hatua zitachukuliwa kwa kufuata katiba, kanuni,
maadili, itifaki na miongozo ya chama.
*Aron J
Mashuve*
*Mwenyekiti
wa BAVICHA*
*Mkoa Wa
Tanga
NAPENDA
kutoa taarifa kwa umma kutokana na habari zinazoandikwa kwenye baadhi ya vyombo
vya habari, huku chanzo cha habari hizo kikiwa ni Katibu wa BAVICHA Mkoa wa
Tanga, Bwana Deogratias Kisandu, ambazo zimekuwa zikionesha kuwa vijana wa Mkoa
wa Tanga tuna walakini katika chama chetu cha CHADEMA.
Leo
katika baadhi ya vyombo vya habari, Bwana Kisandu amenukuliwa akitoa taarifa
kuwa yeye pamoja na makatibu wenzake nchi nzima, wamepanga kufanya maandamano
ya kuupinga uongozi wa juu wa kitaifa wa BAVICHA.
Kwa
kutambua na kuheshimu kuwa moja ya misingi muhimu ya uendeshaji wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na mabaraza yake ni vikao, ambavyo
vipo kwa mujibu wa Katiba, miongozo, taratibu, kanuni na itifaki za chama,
vijana wa CHADEMA Mkoa wa Tanga, ambao mimi ndiye msemaji wao kikatiba,
tunaamini Bwana Kisandu anazidi kupotoka.
Kwa hiyo
basi, kama ambavyo nimeshapokea malalamiko kutoka kwa vijana wa Tanga baada ya
hatua yake ya awali ya Bwana Kisandu kutoa taarifa kwa vyombo vya habari, bila
kuzingatia katiba, maadili na itifaki ya chama, akibeba propaganda nyepesi za
Sekretarieti ya CCM, juu ya suala la kadi mbili kwa Katibu Mkuu wetu Dkt.
Willibrod Slaa, kuna haja ya kufanya vikao kuangalia na kujadili mwenendo wa
kiongozi mwenzetu huyo.
Kwa sababu kama vijana makini wa CHADEMA, chama ambacho kinaamini katika kutoa utumishi bora, mikakati madhubuti, sera imara kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Watanzania wote, ambao wamekosa uongozi bora na siasa safi kutokana na ufisadi na ubadhirifu wa CCM, lazima tuwe makini na kila mwenzetu yeyote yule ambaye anaonekana kufanya kazi ya CCM kwa kutumia jina la CHADEMA.
Tunapenda kumkumbusha Bwana Kisandu kuwa atumie muda wake pia kuisoma vyema
katiba ya CHADEMA hasa katika Sura ya 10 inayozungumzia Maadili ya Viongozi, Sifa mahususi za viongozi na maadili ya wanachama, kifungu
10.1(1-13), toleo la mwaka 2006.

Post a Comment