Na Hamisi Mohamedi-
Morogoro
Waziri wa mawasiliano
nchini Prof.Makame Mbarawa amefungua kikao cha pili cha mamlaka ya mawasiliano
nchini TCRA kilichofanyika jijini Dar es salam.
Akizungumza katika ufunguzi
huo Prof. Mbarawa amesema serikali imejipanga vyema katika kukabiliana na
mabadiliko ya kutoka katika mfumo wa Analogy na kwenda Digital.
Prof. Mbarawa amewataka
mawakala walioidhinishwa na mamlaka hiyo ya mawasiliano nchini TCRA wazingatie
ubora wa matangazo kama inavyotarajiwa na wengi.
Pia kwaupande wa wamiliki
wa nyombo vya habari Pro. Mbarawa amewataka wamiliki hao kujikita katika
kutayarisha vipindi vya kuelimisha jamii hasa jamii ilioko vijijini ambayo ndio
kundi kubwa la watanzania wapo huko.
Mkutano huo wa siku mbili
ulikuwa na lengo lakuwakumbusha wamiliki wa vyombo vya habari na waandaaji wa
vipindi waandae vipindi vya kuielimisha jamii
Post a Comment