Reli ndefu kabisa
duniani ya treni ya kasi leo imezinduliwa rasmi. Reli hiyo yenye umbali wa
kilomita 2298 inaunganisha mji mkuu Beijing na Guangzhou, mji muhimu wa biashara
kusini mwa China inafupisha muda wa usafari hadi saa 7 na dakika 59 kutoka zaidi
ya saa 20 na nusu.
Saa 3 leo asubuhi treni
ya kwanza ya kasi iliondoka Beijing, kaskazini mwa China, katika safari ya
kilomita 2298, inapita miji zaidi ya 20 mikubwa kutoka kaskazini hadi kusini mwa
China, na kufika mwisho wa reli hiyo, mji wa Guangzhou. Katika safari ya
majaribio iliyofanyika jumamosi iliyopita, treni iliendeshwa kwa kasi ya wastani
ya kilomita 300 kwa saa.
Bei ya tiketi ni kutoka
Yuan 865, dola 140 za kimarekani hadi Yuan 2727, sawa na dola 450 za kimarekani.
Si bei rahisi, lakini kutokana na kasi yake, hali ya juu ya usalama ya safari za
treni, na kivutio cha teknolojia za hali ya juu za treni ya kasi, tiketi za
treni zote za leo zimeuzwa kabisa. Ofisa wa kituo cha reli cha Beijing alisema
treni ya kwanza ina viti 1051, tiketi zote ziliuzwa na abiria wengi wanakwenda
Guangzhou kutalii au kuwatembelea jamaa zao.
Bibi Li ni abiria wa
treni hiyo ya kwanza. "Hii ni reli ndefu kabisa ya treni ya kasi nchini China na
duniani. Nafurahi sana nimeweza kununua tiketi ya treni yake ya kwanza. Nasikia
salama zaidi kusafiri kwa treni kuliko ndege. Bei yake ni kubwa kweli, lakini
nasikia salama."
Wizara ya reli ya China
imechukua hatua kadhaa za kuhakikisha usalama wa safari, zikiwemo kuimarisha
shughuli ya marekebisho ya vifaa vya kudumu na vifaa vya mikononi ndani ya treni
, na kuboresha mfumo wa udhibiti ili kushughulikia matatizo yanayoweza
kusababishwa na hali mbaya ya hewa.
Wachina watasherehekea
mwaka mpya wa jadi mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka 2013. Katika kipindi cha
sikukuu hiyo muhimu zaidi kuliko nyingine katika jamii ya wachina, mamilioni ya
watu watasafiri nchini China, na safari za treni ni njia kuu ya mawasiliano.
Uzinduzi wa reli hiyo ya treni ya kasi inatarajiwa kupunguza msongamano wakati
wa sikukuu hiyo.
Mbali na kuongeza uwezo
wa uchukuzi wa reli nchini China, reli hiyo ya treni ya kasi pia inayopita
maeneo kadhaa muhimu ya kiuchumi inatarajiwa kuchangia mambo ya uchumi na
biashara. Imefahamika kuwa hadi mwaka 2015 reli hiyo itarefushwa hadi Hong
Kong.

Post a Comment