Ridhiwani
Kikwete.
Assah
Mwambene |
MAANDALIZI
ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
yanaenda vizuri na wajumbe wanatarajiwa kufika Bagamoyo Ijumaa Desemba 28, 2012
mchana kwenye hoteli ya Kiromo View Resort watakapolala na kufanyia
mkutano.
Washiriki watatembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria Bagamoyo na jioni
kutakuwa na mechi ya kirafiki kati ya timu ya soka ya TASWA FC na Bagamoyo
Veterani itakayofanyika Uwanja wa Mwanakalenge na usiku wajumbe watakuwa na
chakula cha pamoja na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali
yahusiyo michezo na taaluma ya habari.
Mkutano
Mkuu utafunguliwa Jumamosi Desemba 29, saa tatu asubuhi na mgeni rasmi atakuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Kusaidia timu za Taifa za Vijana, Ridhiwani
Kikwete.TASWA imechukua jukumu la kumualika kutokana na kuwa mdau mkubwa na
rafiki wa chama chetu.
Mkutano
utafungwa jioni na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah
Mwambene ambaye hiyo pia itakuwa nafasi nzuri kwake kuweza kuzungumza na wana
habari kuhusiana na masuala mbalimbali ya kitaaluma.
Katika mkutano huo wanachama wa
TASWA watapata fursa ya kupokea na kujadili Ripoti ya Utendaji ya chama, Mapato
na Matumizi, maendeleo ya chama na masuala mbalimbali yanayohusu waandishi wa
habari za michezo na maendeleo ya michezo kwa ujumla Pia kutakuwa na semina maalum
itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo, ili wawe na uelewa kuhusiana na
ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama ambayo nayo itajadiliwa kwenye mkutano
huo.
Kamati ya
Utendaji ya TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze kujitegemea kwa
kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini imeamua kwanza iwaite
wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya jambo hilo na kukishakuwa na
uelewa wa kutosha suala hilo litakuwa kama ajenda kamili ya kuanzisha chama
hicho kwenye mkutano wetu.
Amir
Mhando
Katibu Mkuu
TASWA
Post a Comment