Pambano la kirafiki la
kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zambia (Chipolopolo) lililochezwa
juzi (Desemba 22 mwaka huu) limeingiza sh. 109,197,000.
Fedha hizo zimepatikana
kutokana na watazamaji 17,383 waliokata tiketi kushuhudia mechi kwa kiingilio
cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh.
30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo
ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh.
16,657,169.49, maandalizi ya mchezo sh. 55,339,510, tiketi sh. 5,803,900, ulinzi
na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000, Wachina (technical support) sh.
2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh.
400,000.
Nyingine ni bonasi kwa Taifa
Stars sh. 13,826,313, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 2,504,022, asilimia
10 ya uwanja sh. 1,252,011, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) sh. 626,005 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh.
8,138,070.
Mapato ya mechi nyingine
za Taifa Stars ilizocheza nyumbani mwaka huu yalikuwa Taifa Stars vs Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo-DRC (Leopards) iliyofanyika Februari 23 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam sh. 32,229,000. Taifa Stars vs Msumbiji (Mambas)
iliyochezwa Februari 29 mwaka huu sh. 64,714,000.
Taifa Stars vs Malawi
(The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
iliingiza sh. 40,980,000. Taifa Stars vs Gambia (The Scorpions) iliyochezwa Juni
10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zilipatikana sh. 124,038,000 na
Taifa Stars vs Kenya (Harambee Stars) iliyofanyika Novemba 14 mwaka huu Uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza iliingiza sh. milioni 45.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)
Post a Comment