Taifa Stars |
Na Prince
Akbar wa Bin Zubeiry
TIMU ya soka
ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo inashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kumenyana na mabingwa wa Afrika, Zambia ‘Chipolopolo’ katika mchezo wa
kujipima nguvu kabla ya kwenda kutetea Kombe lao nchini Afrika Kusini mapema
mwakani.
Zambia
imetua nchini na wachezaji 24, maofisa wengine wanane wakiwemo wa benchi la
ufundi linaloongozwa na Kocha Mfaransa, Herve Renard aliyeipa timu hiyo ubingwa
wa Afrika mwaka jana nchini Gabon.
Wachezaji
waliokuja na Zambia ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo,
Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na
Francis Kasonde.
Wengine ni
Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga,
Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga,
Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila
Sunzu.
Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Dar es Salaam
tangu Desemba 12 mwaka huu chini ya Kocha Mdenmark, Kim Poulsen kujiandaa kwa
mechi hiyo.
Viingilio
katika mechi ya leo vitakuwa Sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani,
Sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, Sh. 10,000 kwa VIP C, Sh. 20,000 kwa
VIP B wakati VIP A itakuwa Sh. 30,000.
Tiketi
zilianza kuuzwa tangu jana katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa,
Uwanja wa Uhuru, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni
Kariakoo, kituo cha mafuta cha Ubungo OilCom na Dar Live
Mbagala.
Mara ya
mwisho ilipojitupa dimbani Novemba 14, mwaka huu Stars iliibuka na ushindi wa
bao 1-0 dhidi ya Kenya, Harambee Stars kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza
katika mchezo wa kirafiki, ambalo lililotiwa kimiani na beki Aggrey Morris
katika dakika ya nne, baada ya kupanda kusaidia
mashambulizi.
Hii itakuwa
mechi ya tisa kwa Stars mwaka huu, nane za awali, ikishinda mbili moja ya
mashindano na moja ya kirafiki, kufungwa moja na sare
tano.
Iliifunga
2-1 Gabon katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia
kabla ya kuifunga Kenya 1-0.
REKODI YA
STARS MWAKA HUU NA RATIBA YA MECHI ZIJAZO:
Februari 23,
2012
Tanzania 0 –
0 DRC (Kirafiki)
Februari 29,
2012
Tanzania 1 –
1 Msumbiji (Kufuzu Mataifa ya
Afrika)
Mei 26,
2012
Tanzania 0 –
0 Malawi
Juni 2,
2012
Ivory Coast
2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la
Dunia)
Juni 10,
2012
Tanzania 2 –
1 Gambia (Kufuzu Kombe la
Dunia)
Juni 17,
2012
Msumbiji 1 –
1 Tanzania (Tanzania ilitolewa kwa penalti kufuzu Mataifa ya
Afrika)
Agosti 15,
2012
Botswana 3 –
3 Tanzania (Kirafiki)
Novemba 14,
2012
Tanzania 1-0
Kenya (Kirafiki)
Desemba
22, 2012
Tanzania Vs
Zambia (Kirafiki)
MECHI
ZIJAZO
Machi 22,
2013
Tanzania Vs
Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 7,
2013
Morocco Vs
Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 14,
2013
Tanzania Vs
Ivory Coast (Kufuzu Kombe la
Dunia)
Septemba 6,
2013
Gambia Vs
Tanzania (Kufuzu
Kombe la Dunia)
Post a Comment