Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAIFA STARS YAIBUKA MSHINDI KWA GOLI 1 KWA BILA DHIDI YA TIMU YA ZAMBIA


 

Hivi ndivyo Usomekavyo Ubao wa Matokeo katika Uwanja huu wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa kipindi cha kwanza cha mchezo katika ta Taifa Stars na Mabingwa wa Afrika,Zambia wana Chipolopolo.kipindi cha kwanza kimemalizika sasa huku Taifa Stars ikiongoza kwa bao moja lililotiwa kimiani na Mrisho Ngassa mnamo dakika 45 ya mchezo kipindi cha kwanza.
Mshambuliaji wa Taifa Stars,Hamis Mcha (katikati) akiwachachafya mabeki wa timu ya Zambia katika mchezo wa kirafiki unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa stars imeshinda goli 1-0.
Hamis Mcha (7) akiendelea kuwapa kazi mabeki wa timu ya Zambia.
Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akiingia kwenye lango la timu ya Taifa Stas,huku beki wa Stars,Aggrey Moris akijiandaa kukabiliana nae.
Mchezaji wa timu ya Zambia,Moses Phiri (9) akijaribu kutaka kumtoka beki wa Taifa stars,Salum Aboubakar wakati wa Mchezo wa Kirafiki unaoendelea hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Taifa stars wanaongoza kwa bao moja lililotiwa kimiani na Mshambuliaji machachari,Mrisho Ngassa mnamo dakika ya 45 ya mchezo.
Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog
**************
Na Prince Akbar wa Zubeiry Blog
KAMA ingekuwa ni ndondi, leo Tanzania wangetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Afrika, baada ya kuwapiga Zambia, lakini katika soka, haiku hivyo.
Tanzania, Taifa Stars leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika michezo ya kirafiki baada ya kuifunga Zambia 1-0, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Stars ambayo Novemba 14, mwaka huu iliifunga 1-0 Kenya, Uwanja wa CCM Kirumba, walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa.
Ngassa, anayecheza kwa mkopo Simba SC akitokea Azam FC, zote za Dar es Salaam, alifunga bao hilo dakika ya 45, akimalizia pasi nzuri ya kiungo wa Simba SC, Mwinyi Kazimoto.
Stars ilicheza vizuri na kwa umakini wa hali ya juu kipindi cha kwanza, na kufanikiwa kuwabana mabingwa hao wa Afrika wanaojiandaa kwenda kutetea taji lao nchini Afrika Kusini mapema mwakani.
Kipindi cha pili, Zambia walianza kwa kurekebisha kikosi chao, kocha Mfaransa, Herve Renard akiwatoa Hichani Himonde, Moses Phiri, Sinkala na Isaac Chansa na nafasi zao kuchukuliwa na Stopila Sunzu, Mukuka Mulenga, Evans Kangwa na Francis Kasonde.
Pamoja na mabadiliko hayo, Stars iliendelea kung’ara na katika dakika ya 57 Ngassa alikaribia kufunga tena kama si shuti lake kufuatia pasi ‘tamu sana’ ya Sure Boy kutoka nje.
Lakini kukosa kwa Ngassa bao hilo, kulitokana na maarifa ya beki wa TP Mazembe ya DRC, Stopila Sunzu anayejiandaa kuhamia Reading ya England, ambaye alimbana kiungo huyo wa Simba kumynima mwanya wa kupiga vizuri na akafanikiwa kumfanya apige nje.
Zambia walipoteza nafasi nzuri ya kusawazisha bao dakika ya 76, baada ya shuti la Chasamba Lungu kugonga mwamba, wakati kipa Juma Kaseja akiwa amekwishapotea maboya.
Ngassa alijibu shambulizi hilo dakika ya 77 baada ya shuti alilojaribu kupaa juu ya lango, huku Felix Katongo akipewa kadi ya njano, baada ya kumuangusha Amri Kiemba aliyekuwa anamfunga tela.
Juma Kaseja alifanya kazi ya ziada dakika ya 86, baada ya kuokoa shuti la karibu la Chris Katongo na katika dakika ya 87, Stars ilipata pigo baada ya beki Kevin Yondan kuumia na nafasi yake kuchukuliwa beki mwenzake wa Yanga, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ dakika ya 88.
Kikosi cha Stars leo kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kevin Yondan/Nadir Haroub dk 87, Frank Domayo, Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa/Amir Maftah dk83 na Khamis Mcha ‘Vialli’/Simon Msuva dk59.
Zambia; Danny Munyao, Chintu Kampamba, Hichani Himonde, Chisamba Lungu, James Chamanga, Moses Phiri, Chris Katongo, Felix Katongom Nathan Sinkala/, Rodrick Kabwe na Isaac Chansa. 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top