Louise
Kamin Meneja Mradi wa Media For Development International Tanzania akizungmza
kuelezea filamu ya Siri ya Mtungi ilyotengenezwa na taasisi hiyo itakayokuwa
ilirushwa na vituo vya televisheni vya ITV na EATV ikiwa na maudhui ya maisa
katika familia ya jamii
inayohamasishwa na penzi, lililoletwa na woga, ushirikina na usaliti,
ikinyanyuliwa na ucheshi na furaha, na kupewa nguvu ya mshikamano wa
ndani wa familia na urafiki. Uzinduzi wa filamu hiyo ulifanyika jana kwenye
ofisi za shirika hilo Msasani jijini Dar es salaam
Baadhi ya waandishi wa
habari na wageni walioalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika ofisi za
shirika hilo Msasani jijini Dar es salaam.
Baadhi ya
washiriki waliocheza katika filamu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
ya uzinduzi huo jana.
………………………………
Tamthilia mpya kabisa ya
Televisheni kutoka kwa Watu wa Marekani! Onyesho la Kwanza la SIRI
YA MTUNGI litakuwa
ITV saa 3.30 usiku tarehe
9 Desemba. Na EATV saa 3.30 usiku tarehe 12
Desemba.
Mchanganyiko mzuri wa
wahusika wa Siri
ya Mtungi, waliohusiana kwa damu au ndoa, au kwa mapenzi tu,
unaunda
jamii inayohamasishwa na
penzi, lililoletwa na woga, ushirikina na usaliti, ikinyanyuliwa na
ucheshi na furaha, na
kupewa nguvu ya
mshikamano wa ndani wa familia na urafiki.
Tamthilia hii ya
Televisheni ni Programu ya awali ya TCCP (Tanzania Communications
Capacity Project) iliyotekelezwa
na JHU-‐CCP (Johns
Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communications
Programs) kwa msaada
wa USAID (United States
Agency for International Development) na kama sehemu ya PEPFAR (US
President’s
Emergency Fund for AIDS
Relief).
Ikiwa imetayarishwa na
MFDI (Media For Development International), Siri
ya Mtungi inawaleta pamoja Wasanii bora
wa Tanzania, waandishi,
wana mitindo ya nguo, wakurugenzi wa sanaa, waigizaji na watendaji wa
filamu kwenye
mafanikio makubwa ya
ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni Tanzania.
Kati ya mitaa yenye
harakati nyingi ya Dar es Salaam na ile iliyo kimya ya Bagamoyo,
tunapenya nyuma ya milango
iliyofungwa mpaka kwenye
maisha ya Cheche na mkewe Cheusi, binti wa kiongozi maarufu katika
jamii, mwenye
wake wengi, Mzee Kizito,
pamoja na wahusika wengine kama Duma, mwana DJ; Lulu-‐ shangingi
lililokubuhu; Farida-‐
roho ya nyoka;
Masharubu-‐ mzee kikwekwe na wengine wengi.
RATIBA YA ITV: Jumapili
3.30 usiku -‐ Jumatano 3.30 usiku
RATIBA
YA EATV: Jumatano 10.30 Alasiri -‐ Alhamisi 7.00 Mchana
-‐ Jumamosi 10.30 Alasiri
Post a Comment