Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House na
Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania Red ribbon Fashion Gala,Khadija
Mwanamboka (kulia) akikabidhi cheti kwa Mwanamitindo Maarufu nchini,Flaviana
Matata ambaye ni Muanzilishi wa taasisi ya kusaidia jamii iliyo kwenye matatizo
ya Flaviana Matata Foundation,wakati wa kuadhimisha Miaka Mitano ya Onyesho la
Mavazi la Tanzania Red Ribbon Fashion Gala ambalo hufanyika Desemba 1,kila mwaka
ikiwa ni kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani,lililofanyika kwenye Hoteli ya
Serena,jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa
Tanzania Mitindo House na Muandaaji wa Onyesho la Mavazi la Tanzania Red ribbon
Fashion Gala,Khadija Mwanamboka (kulia) akikabithi Cheti kwa Dada Halima
Rashid.
Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House na Muandaaji
wa Onyesho la Mavazi la Tanzania Red ribbon Fashion Gala,Khadija Mwanamboka
(kulia) akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi wa Hoteli ya Giraffe,Dk. Charles
Beccon.
Wanamitindo wakipita jukwaani kuonyesha mavazi
mbali mbali yaliyobuniwa na Wabunifu wa hapa nchini.
Waendeshaji wa Onyesho hilo,Evans Bukuku (picha
ya juu) na Abby wakionyesha nao umahiri wao wa kutembea jukwaani kwa mwendo wa
kiuana Mitindo.
Mwanamitindo Maarufu nchini,Flaviana Matata
(kushoto) ambaye ni Muanzilishi wa taasisi ya kusaidia jamii iliyo kwenye
matatizo ya Flaviana Matata Foundation akiongoza mnada wa nguo walizozivaa kwa
ajili ya kukusanya hela ya kusaidia wahitaji walio chini ya Taasisi hiyo,ambapo
hadi mnada wa vitu mbali mbali unamalizika jumla ya shilingi Milioni 72 ziliweza
kukusanywa hiyo jana.Kulia ni Mwanamitindo,Jenuffer
Bash.
Wadau wakifatilia kwa Umakini Onyesho
hilo.
Post a Comment