Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TUWE MAKINI NA BODA BODA

JUMLA ya pikipiki za miguu miwili maarufu kama bodaboda 1,717 zimesababisha ajali zilizoua watu 138 wakiwa ni wananume 132 na wanawake sita Pia pikipiki 276, zimekamatwa kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kusababisha ajali.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa majeruhi baadhi yao wamepata ulemavu wa kudumu na wengine wako hospitali mpaka sasa hali inayotishia usalama wa maisha na mali za wananchi.
Alisema ajali hizo nyingi zinasababishwa na kutovaa kofia ngumu, kuendesha bila leseni, ubovu wa pikipiki, mwendokasi na kupakia abiria zaidi ya mmoja.
Kova alisema madereva wengi wa pikipiki wameshindwa kujua sheria kifungu namba 14 cha kanuni za Sumatra ambacho hakiruhusu watoto chini ya miaka tisa kupakizwa kwenye usafiri huo.
Alisema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na Sumatra litahakikisha sheria zote za barabarani zinafuatwa ili kuondoa kero hizo.



Chanzo: Tanzania Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top