Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Uchunguzi wa Afya sasa hapahapa, safari za India basi - NSSF


MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau(Pichani), ametangaza neema kwa Watanzania., kuwa kufikia Februari mwakani, wagonjwa waliokuwa wanapelekwa nchini India kwa uchunguzi wa afya, sasa wataanza kuhudumiwa hapa nchini.

“Napenda kuwaambia Watanzania, ifikapo Februari mwakani wataanza kupata huduma za uchunguzi wa afya, badala ya kwenda nchini India kama ilivyozoeleka, hii ni habari njema,” alisema Dk. Dau.
 

Alisema hali hiyo, imefikiwa baada ya kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambayo tayari wameingia mkataba na Hospitali ya Apollo ya India, ambayo itafunga mitambo ya kisasa ya kuchunguza afya na kufanya matibabu ya msingi katika Jengo la NSSF, lililopo eneo la barabara ya Bibi Titi Mohamed, mjini Dar es Salaam.

“Pale Bibi Titi Mohamed, tuna jengo letu ambalo tumeamua kuchukua ghorofa tatu za chini na vifaa vyote vya kisasa vimeanza kufungwa, hatuoni sababu ya mtu kuhangaika kumsafirisha mgonjwa kwenda kupata uchunguzi wa vipimo India.

“Vifaa hivi vitatumiwa kufanya uchunguzi wa afya kuanzia kichwani hadi kwenye kisigino. Hatutakuwa na sababu tena ya kumpeleka mtu India, kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya, labda kwa magonjwa yaliyoshindikana tu,” alisema Dk. Dau

Alisema uongozi wa Hospital ya Apollo, umepewa maelekezo ambayo yanaitaka kutotoza gharama kubwa za matibabu.

“Kwa mfano kama mtu aliwahi kupima kipimo cha mwili mzima, kinachogharimu dola 200 (Sh 360,000) India, ni wazi hapa gharama zitapungua tu, nasema hivyo kwa sababu kila Mtanzania anastahili kupata huduma kwa gharama nafuu, kutokana na kipato chake,” alisema Dk. Dau.

Kwa miradi hii iliyotajwa ikikamilika, Jiji la Dar es Salaam litabadilika sura na kuwa la kisasa sawa na majiji mengi duniani ya nchi zilizoendelea.

Naye, Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika hilo, Yacoub Kidula, alisema mfuko umeanzisha mradi wa kujenga nyumba za kisasa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

Alisema mradi huo, umelenga kujenga nyumba za dharura kwa Watanzania, watakaohamishwa katika maeneo yao ambako zitajengwa nyumba za kisasa na baadaye watarudishwa kwenye makazi yao.

Mtanzania
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top