Afisa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akitoa muhtsari kwa
waandishi wa habari juu ya Taarifa kuhusu Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Msaada
wa Maendeleo UNDAP 2011-2015 ambao unaelezea ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika
kuendeleza nyanja mbalimbali ikiwemo kupunguza umaskini wakati wa Semina ya
kuwapa uelewa waandishi wa habari juu ya Haki za Binadamu tukielekea kwenye
maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani itakayoadhimishwa tarehe 10
Disemba mwaka huu.
Mwezeshaji
wa Semina hiyo Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini Neville Meena akitoa
changamoto kwa wanahabari kutumia fursa mafunzo hayo katika kuhabarisha jamii
kuhusu kazi zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa
nchini.
Mwakilishi
Msaidizi wa UNICEF Bw. Paul Edwards akielezea nia ya Umoja wa Mataifa
kuwakutanisha waandishi wa habari kila mwaka katika semina za mafunzo ambapo
amesema jitihada za Umoja huo kutoa mchango katika juhudi endelevu za kupunguza
umaskini na kupatikana kwa haki za Binadamu kulingana na visheni ya Maendeleo ya
Taifa la Tanzania.
Mtalaam wa
Program wa UNDP Bw. Amon Manyama akiwasilisha kwa wanahabari mpango kazi maalum
wa miaka minne unaojulikana kama United Nations Development Assistance Plan
2011-2015 (UNDAP) uliotenga dola za Kimarekani Milioni 777 kwa Serikali ya
Tanzania mpaka kukamilika ifikapo 2015.
Mratibu wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yasiyo na ukazi hapa nchini Bi. Aine Mushi
akizungumzia jinsi mashirika hayo yanvyoweza kufanya kazi kwa pamoja 'Delivering
As One' na Mashirika ya Umoja wa mataifa yenye ukazi hapa
nchini.
Pichani Juu
na Chini ni Washiriki wa Semina ya siku moja kutoka vyombo mbalimbali vya habari
hapa nchini.
Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mh. Mahfoudha Alley Hamid
akizungumzia haki za msingi za Binadamu na wajibu wa vyombo vya habari katika
kutetea haki hizo na kufichua pale zinapokiukwa ikiwemo kufuata
maadili.
Afisa
Mipango Mwandamizi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bw. Anthony Rutabanzibwa
akitoa somo jinsi waandishi wa habari wanavyotakiwa kuripoti masuala yanayohusu
hakiza Binadamu bila kutoka nje maadili ya kazi zao.
Pichani Juu
na Chini ni baadhi ya washiriki wakichangia mada na kutoa maoni wakati wa semina
hiyo.
Mwenyekiti
wa timu ya Mawasiliano ya Umoja Mataifa Bw. Yusuph Al Amin wakati wa semina hiyo
akifafanua jinsi sekta ya mawasiliano vikiwemo vyombo vya habari inavyoweza
kuchangia maendeleo na kufanikisha kufuatwa kwa haki za
binadamu.
Afisa
habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama akitoa
changamoto kwa wanahabari kusoma makabrasha yanayotolewa na mashirika mbalimbali
ya umoja wa mataifa wakati wa mikutano na semina za kuelimishana kuhusiana na
masuala mbalimbali yanayohusu jamii kwani kwa kufanya hivyo ndivyo
watakavyoeweza kuelewa ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika kupunguza umaskini na
kutetea haki za binadamu.
Baadhi ya
Maofisa wa Umoja wa Mataifa na Wanahabari wakati wa Semina hiyo.
Post a Comment