Na Elizabeth
John
NTOTA wa muziki wa kizazi
kipya nchini, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ amaeachia video ya wimbo wake mpya
unaokwenda kwa jina la ‘Utamu’ amabao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali
vya redio.
Akizungumza na Habari Mseto
jijini Dar es Salaam, Dully alisema wimbo huo kawashirikisha wakali wa muziki
huo, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ na Omary Faraji ‘Ommy Dimpoz’ ambao
anaamini wamefanya vizuri katika wimbo huo.
“Niliamua kuwashirikisha
wasanii hao kwasababu wanafanya vizuri na wanakubalika katika ‘game’, naamini
uwepo wao utakuwa wa mafanikio makubwa kwangu pamoja na burudani kwa mashabiki
wa muziki huo,” anasema Dully.
Anasema wimbo huo umeanza
kuonekana katika vituo mbalimbali vya redio wiki hii, anawaomba mashabiki wake
wampokee vizuri na kwamba wasikae mbali nay eye kuna vitu vingi ambavyo
amewaandalia.
Mbali na kutaka kutoka na
kibao hicho, Dully alishawahi kutamba na nyimbo zake kama Mtoto wa Kariakoo,
Dhahabu na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika muziki wa
bongo fleva.



Post a Comment