Akizungumza na waandishi wa habari jana wilayani hapa, Mwenyekiti wa umoja huo, Solomoni Mataba, alisema wamedhamiria kuwang’oa katika nafasi zao watumishi wasio waadilifu, wanaochangia kuipaka matope serikali iliyopo madarakani.
Alisema kuwa wamejipanga kuwafichua wasiofuata maadili ya uwajibikaji kazini na kuwa kero, ikibidi kwa kufanya maandamano ili wakazi wa wilaya hiyo waweze kupata haki yao.
Mataba aliwataka watumishi waliosahau wajibu wao huku wakijifanya miungu watu, kuhakikisha wanafuata maadili na kuacha kufuata maslai binafsi ambayo imekuwa sababu kubwa ya jamii kuichukia serikali.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa baadhi ya idara zimejisahau, huku zikiwanyanyasa wananchi hatua ambayo inazidisha chuki kwa serikali yao.
chanzo: Tanzania Daima
Post a Comment