SERIKALI imetoa siku 30 kwa wananchi
wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha kabla hawajachukuliwa hatua
za kisheria.
Kauli hiyo
imetolewa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.
Emmanuel Nchimbi wakati akizungumza na waandishi wa
habari
Dkt. Nchimbi
alisema kuwa na tatizo la kuzagaa na matumizi holela ya silaha zinazomilikiwa
isivyo halali lichangia matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakijitokeza
sehemu mbalimbali nchini.Alisema kuwa kwa mfano katika mwezi
Januari hadi Septemba mwaka huu kumekuwepo na matukio ya ujambazi 876 ambayo
yalisababisha vifo 138 vya raia na 6 vya askari.
Aidha Dkt .
Nchimbi aliongeza kuwa jumla ya mali zenye thamani ya shilingi
bilioni 4.5 zilizoibiwa kwa kutumia silaha zinazomilikiwa kinyume
cha sheria na zile zinazomilikiwa kisheria lakini wamiliki wake wanazitumia
katika uhalifu.
Aliongeza kuwa kipindi cha kuanzia Januari hadi
Septemba mwaka huu jumla ya silaha 62 ziliibiwa kutoka kwa wamiliki wake halali
na silaha 304 zilikamatwa katika matukio mbalimbali ya uhalifu Kufuatia hali
hiyo Serikali imewaagiza watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha Sheria
kusalimisha silaha hizo katika vituo vya Polisi au wenyeviti wa vitingoji ,
wakuu wa mikoa na wilaya.Aidha Dk. Nchimbi alisema kuwa kwa wale ambao muda
utakamailka bila kusalimisha silaha msako mkali utafanyika kuanzia tarehe 5
Januari mwakaniWaziri Nchimbi aliwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya dola
kutoa taarifa zitakazosaidia kubaini uhalifu na makundi yaliyo katika jamii
yetu
Post a Comment