Mhandisi Zablon Mafuru (kulia) ambaye ni mkuu wa Kituo cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mwanza akimuonyesha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) hivi karibuni mtambo wa redio Tanzania wa masafa marefu (Medium Wave) unaorusha matangazo yake katika mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Shinyanga, Kigoma , Siminyu na nchi jirani za Uganda na Rwanda uliopo Ilemela jijini Mwanza.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akiangalia mtambo wa
kurushia matangazo ya redio kwa masafa mafupi (Short Wave) na Televisheni wa
Shirika la Habari la Tanzania (TBC) hivi karibuni uliopo eneo la Nyashana jijini
Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana James
Kajugusi.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akikagua hivi karibuni
kiwanja cha Shirika la Habari la Tanzania (TBC) kilichopo eneo la Kapripointi
jijini Mwanza. Kulia ni Eston Sanga ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa Shirika
hilo.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akiongea jambo hivi
karibuni na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Habari la Tanzanzani (TBC) mara
baada ya kumaliza ziara yake fupi ya kutembelea ofisi za kanda ya Ziwa za
shirika hilo zilizopo jijini Mwanza. Kulia ni Eston Sanga ambaye ni Mkuu wa
Kanda ya Ziwa wa Shirika hilo na wapili kushoto ni Mhandisi Zablon Mafuru
ambaye ni mkuu wa Kituo cha Mwanza akifuatiwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka
Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (aliyevaa suti ya dark
blue).
Mhandisi Zablon Mafuru (kulia)
ambaye ni mkuu wa Kituo cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akimuonyesha
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wa pili
kulia) mtambo wa kurusha matangazo Televisheni kwa njia ya digitali (haupo
pichani) uliopo eneo la Nyashana jijini Mwanza. Kuanzia tarehe moja mwezi wa
kwanza mwaka 2013 vituo vyote vya Televisheni vitarusha matangazo yake kwa njia
ya digitali.
Picha na Anna Nkinda –
Maelezo
Post a Comment