WAZIRI MKUU Mizengo
Pinda ameahidi kutoa trekta moja kwa ajili yakikundi cha vijana katika kata ya
Ilunde ili waweze kuondokana na kilimo cha jembe la mkono na waboreshe uchumi wa
eneo hilo.mAmetoa ahadi hiyo leo (Ijumaa, Desemba 14, 2012), wakati
akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ilunde kwenye uwanja wa shule ya msingi
Ilunde katika siku ya pili ya ziara yake jimboni kwake Katavi wilayani
Mlele,
mkoani
Katavi.
Waziri Mkuu ambaye ni
mbunge wa jimbo la Katavi alisema atawapatia trekta hilo kama mkopo ili nao
wakirudisha trekta jingine, liweze kukopeshwa kwa kikundi kingine. “Hapa
naanzisha ‘Kopa trekta lipa trekta’. Litakuja likiwa na jembe lake pamoja na
harrow,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
“Ni lazima tuondokane na
kilimo cha jembe la mkono kwa sababu hakina tija… na zaidi nasisistiza
kuondokana na kilimo cha matuta kwa sababu kinatumia nguvu nyingi na kupoteza
eneo kubwa ambalo lingetumika kupanda mazao,” alisisitiza.
Waziri Mkuu alielezwa
matatizo yanayowakabili wakazi hao yakiwemo ubovu wa barabara ya kutoka Inyonga
(km. 60) na ukosefu wa wauguzi wa kike kwa ajili ya akinamama wajawazito. Pia
waliomba kupatiwa minara wa mawasiliano ya simu kwa sababu wanapotaka kupiga
simu, wanalazimika kupanda mti mmoja tu ambao uko km.12 kutoka kijijini
hapo
Akijibu maombi yao,
Waziri Mkuu aliwaita Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpanda na Mhandisi wa Wilaya hiyo
ili watoe maelezo kwa wananchi hao.Kuhusu wauguzi, mganga mkuu wa wilaya hiyo,
Dk. Emmanuel Kamgobe alisema
wanashugulikia suala hilo


Post a Comment