Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto)
akipokea taarifa ya SACCOS ya Ibwera iliyopo wilayani
Bukoba kutoka kwa Benedicta Peter ambaye ni katibu msaidizi. SACCOS
hiyo ilipata
mkopo wa shilingi milioni tano kutoka mfuko wa maendeleo ya vijana na
kuvikopesha vikundi mbalimbali vya maendeleo vya vijana.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wa tatu
kulia) akiangalia jana
nyavu za kuvulia samaki za Kikundi cha Msifuni kilichopo katika kijiji cha
Kemondo wilayani Bukoba ambacho kilipata mkopo kutoka mfuko wa maendeleo ya
vijana na kuanzisha mradi wa bwawa la samaki. Kushoto ni Katibu wa kikundi hicho
Johanes Joel.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (wanne
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa SACCOS ya Ibwera na
viongozi wa wilaya ya Bukoba wakati
alipowatembelea jana ili kuona fedha walizopata kutoka mfuko wa waendeleo ya
vijana zilivyoweza
kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.
Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akiangalia shamba darasa
la kahawa na migomba la mkazi wa kijiji cha Ibwera wilayani Bukoba Ibrahim
Mulokozi (hayupo pichani) wakati alipolitembelea jana ili kuona fedha za
mkopo wa mfuko wa vijana alizozipata kupitia SACCOS ya Ibwera zimemnufaishaje
kimaisha. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi
Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi. Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Post a Comment