Uwanja wa Ndege wa Istanbul ambako Yanga wapo kwa sasa |
Na Mahmoud
Zubeiry wa Bin Zubeiry
YANGA SC,
mabingwa mara tano wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame
wamefika salama Istanbul, Uturuki kiasi cha saa moja iliyopita na sasa
wanasubiri ndege ya kuunganisha kwenda Antalya, ambako wataweka
kambi.
Yanga
itaweka kambi katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa Uturuki na itafikia katika
hoteli ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua
ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na
kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Yanga
iliondoka Dar es Salaam Alfajiri ya leo, saa 10:30 ikiwa na kikosi kamili;
makipa; Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul, mabeki Juma Abdul,
Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Mbuyu Twite,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladisalus Mbogo na Kelvin
Yondani.
Viungo ni
Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin
Bakari, Omega Seme, Simon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende
wakati washambuliaji ni Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerry Tegete, George
Banda na Hamisi Kiiza.
Upande wa
benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts, Kocha Msaidizi Freddy
Felix Minziro na Kocha wa makipa, Razak Ssiwa, na Maofisa wengine ni Daktari wa
timu, Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh, Ofisa Habari, Baraka Kizuguto Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji, Mohammed Nyenge.
Post a Comment