Kufariki
kwa PC Samson kulitokea juzi katika eneo la Mdori mkoani Manyara baada
ya kupata ajali ya gari alilokuwa akilitumia kusafirisha mirungi hiyo
kutoka Arusha.
Taarifa
kutoka vyanzo mbalimbali vya habari eneo hilo la Mdori wilayani Babati
zilieleza jana kwamba ajali hiyo ilitokea saa 12:30 asubihi.
Chanzo
cha habari kilichoshuhudia tukio hilo kilisema kuwa gari hilo liliacha
njia na kuanguka pembeni mwa barabara, hatua iliyosababisha shehena ya
mirungi iliyobebwa kumwagika nje.
Wakati
taarifa kutoka Mdori zikieleza hayo, mtoa taarifa mwingine kutoka
Majengo Kata ya Elerai Arusha alidai kwamba gari hilo lilionekana saa 10
alfajiri likielekea barabara kuu ya Arusha - Babati.
Hata
hivyo chanzo hicho kutoka Arusha nacho kilieleza kwamba shehena hiyo ya
mirungi ilikuwa mali ya mmoja wa wafanyabiashara wa mirungi jijini hapa
(kwa sasa jina linahifadhiwa).
Naye Kamanda wa Polisi Manyara, Akili Mpwapwa alikiri tukio hilo lilitokea saa 12:30 asubuhi eneo la Mdori wilayani Babati.
Alilitaja
gari lililotumika kusafirisha mirungi hiyo kuwa ni Toyota Carrina namba
T. 588 AUW ambalo linadaiwa kuacha njia na kupinduka kutokana na mwendo
kasi.
“Pamoja
na kifo cha PC Samson mtu mwingine anayedaiwa kuwa dereva wa gari hilo
Hussein Bakari (20-30) ambaye ni mkazi wa Arusha naye alifariki dunia
papo hapo.
“Taarifa tulizozipata zinadai kwamba askari huyo alikuwa likizo,” alisema Kamanda Mpwapwa.
Hivi
karibuni Jeshi la Polisi mkoani Arusha lilikamata shehena ya mirungi ya
thamani ya Sh milioni 40 ikiwa imejazwa kwenye gari ya Canter wilayani
Longido.
Iliandikwa Jumamosi, Januari 19, 2013 na Eliya Mbonea wa tanzania Daima, Arusha
Post a Comment