MWENYE wa Muungano wa Afrika, Thomas Boni Yayi, ametoa wito wa kutuma vikosi kusaidia wanajeshi kupambana na makundi ya wapiganaji nchini Mali.
Wapiganaji hao ambao wanajumuisha wale wa Tuareg, wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi.
''Mzozo wa
Mali ulikuwa kitendawili cha kimataifa na NATO inapaswa kusaidia kama ilivyo
saidia Afrghanistan,'' alisema Thomas Boni Yayi.
''Hata
hivyo, harakati dhidi ya wapiganaji hao zinapaswa kuongozwa na kikosi cha
Afrika,'' aliongeza kusema bwana Yayi.
Mwezi jana
Umoja wa Mataifa uliidhinisha mipango ya kutuma takriban kikosi cha wanajeshi
elfu tatu nchini Mali.
''Bila
shaka tuna wasiwasi kuhusu hali na hofu ya kuendelea kuwepo makundi ya kigaidi
katika eneo hilo , inaleta wasiwasi kwa kila mtu kimataifa''.
Maafisa wa
UN wanasema kuwa hawakutarajia wanajeshi hao kutumwa huko kabla ya mwezi
Septemba.
Bwana Yayi,
ambaye ni rais wa Benin,alitoa wito wake baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa
Canada Stephen Harper mjini Ottawa.
"NATO
inapaswa kuchukua jukumu lake katika mzozo huu, na kwamba kikosi cha Afrika
kitatoa mwongozo, sawa tu na hali ilivyokuwa nchini Afghanistan,''
Wanachama
kadhaa wa NATO ikiwemo, Marekani na Ufaransa, wako tayari,kutoa mafunzo kwa
wanajeshi wa Afrika watakaoshiriki katika harakati hizi za kumaliza uasi, ingawa
hawajajitolea kutuma vikosi.
Harper
alisema kuwa Canada , ambayo ni mwanachama wa , Nato, haijatafakari zaidi kuhusu
kujihusisha kijeshi nchini Mali.
Post a Comment