Waziri wa Maliasili na
Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na ujumbe wa wachezaji na waandishi
wa habari kutoka timu ya seattle Sounders ya Canada wakati wa chakula cha jioni
kilichoandaliwa na Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB kwenye hoteli ya serena jijini
Dar es salaam jana kwa ajili ya ugeni huo, Bodi ya Utalii ilisaini mkataba wa
kutangaza utalii wa Tanzania katika kiwanja cha timu hiyo katika ziara
iliyofanywa na Waziri wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki nchini humo katika
msafara huo unaoongozwa na mchezaji wa mpira wa American Football Kevin Griffin
ambaye pia ni Fan Development Marketing wa Sunders FC, wachezaji hao
walitembelea mbuga za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Mbuga ya Tarangire
ambapo walipata muda wa kujionea vivutio vilivyomo katika hifadhi hizo na kupiga
picha
Balozi Khamis Kagasheki
akimsikiliza mmiliki wa timu ya Africa Lyon Rahim Kangezi ambaye ndiye mwenyeji
wa wageni hao wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwenye hoteli ya
Serena Dar es salaam jana, kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mh.
Razalo Nyalandu.
Ugeni huo ukipata chakula
cha jioni katika hoteli ya Serena jana usiku kutoka kulia ni Kevin Griffin
mchezaji wa mpira wa American Footballn Kasey Keller mchezaji maarufu wa mpira
wa miguu vilabu mbalimbali Ulaya na Marekani na mchezaji wa timu ya Taifa ya
MarekaniKristen Addings kutoka Taasisi ya Washington Global Hearthna David Glass
Mtaalam Video na Majarida
Waziri wa Maliasili na
Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Lazaro
Nyalandu katika hafla hiyo kushoto ni Ibrahim Mussa Mkurugenzi wa Utalii Wizara
ya Maliasili na Utalii
Mkurugenzi wa Bodi ya
Utalii Tanzania TTB Dr. Aloyce Nzuki akizungumza na Devotha Mdachi Mkurugenzi wa
Masoko wa Bodi hiyo wakati wa hafla hiyo, katikati ni Mmiliki wa timu ya Africa
Lyon Rahim Kangezi.
Devotha Mdachi Mkurugenzi
wa Masoko Bodi ya Utalii Tanzania TTB akimkaribisha Mh. Waziri Balozi Khamis
Kagasheki na wageni kutoka Seatlle Sounders kwa ajili ya kujitambulisha na
kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa na bodi hiyo.
Kevin Griffin ambaye ndiyo
kiongozi wa msafara huo akimshukuru Mh Waziri na Uongozi wa Bodi ya Utalii TTB
kwa ushirikiano waliouanzisha katika kutangaza utalii wa Tanzania nchini
Canada.
Kasey Keller akizungumza
katika hafla hiyo.
Kasey Keller akimkabidhi
zawadi ya Saa Mh. Lazaro Nyalandu Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii.
Kasey Keller akimkabidhi
zawadi ya saa Ibrahim Musa Mkurugenzi wa Utalii katika Wizara ya Maliasili na
Utalii.
Mh. Waziri Balozi Khamis
Kagashiki akiongozana na Mchezaji wa Seatlle Sounders Marc Burch kuelekea katika
meza ya chakula.
Mh. Lazaro Nyalandu Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji na
waandishi wa habari kutoka Seatlle Sounders nchini Canada pamoja na uongozi wa
Bodi ya Utalii na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Post a Comment