Mustapha Mkulo
BAADHI ya vigogo wa
kisiasa hawatasahau yaliyowapata mwaka jana kutokana na mabadiliko makubwa
yaliyoigusa medani hiyo na kusababisha kuanguka ama kwa kura au kung’olewa
katika nafasi walizokuwa wakizishikilia.
Wakati baadhi wakiugulia
kwa machungu hayo, kwa upande mwingine lipo kundi la wale wanaosherehekea neema
iliyowajia mwaka huohuo, baada ya nyota zao kung’ara kisiasa na kujikuta
wakikwaa nafasi za uongozi, pengine ambazo
hawakuzitarajia.
Miongoni mwa matukio
yaliyowatikisa wanasiasa ni hatua ya Rais Jakaya Kikwete kupangua Baraza la
Mawaziri, kutenguliwa kwa baadhi ya matokeo ya chaguzi za wabunge na uchaguzi wa
ndani wa CCM ambao uliwaweka kando baadhi ya vigogo wa chama
hicho.
Kadhalika, yapo matukio
yenye sura ya kipekee ambayo yanawagusa wanasiasa kama Godbless Lema ambaye
alianguka kisiasa kwa ubunge wake kutenguliwa na Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha
mwanzoni mwa mwaka jana, lakini akaibuka tena shujaa baada ya kurejeshewa nafasi
hiyo na Mahakama ya Rufani, Desemba 2012.
Tukio kubwa ambalo
lilitikisa siasa za Tanzania ni lile la mabadiliko katika Baraza la Mawaziri
ambayo yaliwaweka kando mawaziri sita ambao walikuwa wakiziongoza wizara nyeti
zinazosimamia rasilimali za nchi na huduma za afya na
uchukuzi.
Waliong’olewa ni Mustafa
Mkulo (Fedha), William Ngeleja (Nishati na Madini), Ezekiel Maige (Maliasili na
Utalii), Omari Nundu (Uchukuzi), Dk Cyril Chami (Viwanda na Biashara) Dk Haji
Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii).
Pia panga hilo liliwakumba waliokuwa Naibu Mawaziri, Dk Lucy Nkya (Afya na Ustawi wa Jamii) na Dk Athuman Mfutakamba (Uchukuzi).
Pia panga hilo liliwakumba waliokuwa Naibu Mawaziri, Dk Lucy Nkya (Afya na Ustawi wa Jamii) na Dk Athuman Mfutakamba (Uchukuzi).
Kuanguka kwa Mkulo,
Ngeleja na Maige kulitokana na taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) iliyozihusisha wizara zao na ufisadi.
Dk Mponda na Dk Nkya, waling’olewa kutokana shinikizo la madaktari ambao walifanya mgomo uliotikisa sekta ya afya nchini.
Dk Mponda na Dk Nkya, waling’olewa kutokana shinikizo la madaktari ambao walifanya mgomo uliotikisa sekta ya afya nchini.
Kwa upande wake, Nundu
naibu wake, Dk Mfutakamba waling’olewa kutokana na kashfa ya ujenzi wa gati
bandarini ambao uliwagawa kiasi cha kutofautiana bungeni, wakati Dk Chami naye
aliponzwa na ugomvi na aliyekuwa naibu wake, Lazaro Nyalandu.
Hata hivyo Nyalandu alipona baada ya kuhamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Hata hivyo Nyalandu alipona baada ya kuhamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Walioula
Mabadiliko hayo yalikuwa
neema kwa wateule wapya wakiwamo wale ambao hawakuwahi kuwa wanasiasa kama
ilivyo kwa Profesa Sospeter Muhongo ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na
Madini.
Profesa Muhongo alipewa
naibu wawili; George Simbachawene (Nishati) na Stephen Masele (Madini) ambao
walikuwa wabunge.
Wabunge wengine walioula
ni Dk William Ngimwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na kupewa naibu
wawili ambao nao hawakuwa katika duru za kisiasa; Saada Mkuya Salum na Janeth
Mbene.
Ni wakati huohuo ambao Mwenyekiti wa NCCR -Mageuzi, James Mbatia aliteuliwa na Rais kuwa mbunge.
Ni wakati huohuo ambao Mwenyekiti wa NCCR -Mageuzi, James Mbatia aliteuliwa na Rais kuwa mbunge.
Post a Comment