Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA PILI, 2012 HAYA HAPA

Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Philipo Mulugo ametangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili mwaka 2012, ambapo kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka asilimia 45.40 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 64.55 mwaka 2012.

Matokeo hayo yametangazwa mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo idadi ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 430,327, kati yao wasichana walikuwa 205,476 na wavulana 224,851, ikiwa ni upungufu wa watahiniwa 36,240 ikilinganishwa na mwaka 2011 ambao walikuwa 466,567.
“Watahiniwa 386,271 sawa na asilimia 89.76 ya waliosajiliwa, walifanya mtihani wakiwemo wasichana 187,244 na wavulana 199,027, watahiniwa 44,056 sawa na asilimia 10.24 hawakufanya mtihani, kati yao wasichana ni 18,231 na wavulana 25,825” amesema Mulugo.


Aidha Waziri Mulugo amefafanua kuwa watahiniwa 136,946 ambao wameshindwa kupata wastani wa ufaulu wa alama 30 na wale waliofutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013.
“Ni vema ikaeleweka kuwa kukariri kidato si adhabu bali ni kutoa fursa nyingine kwa mwanafunzi kuweza kupata maarifa, stadi na ujuzi wa elimu ya sekondari, hivyo ni matumaini yangu kuwa wanafunzi hawa watafanya bidii katika kujifunza na kuzingatia masomo ili waweze kufaulu masomo yao katika kiwango kinachotakiwa” amesisitiza Mulugo.
Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili ulifanyika nchini kote kuanzia tarehe 05 Novemba, 2012 na kumalizika tarehe 16 Novemba, 2012 kukiwa na jumla ya vituo 4,304 vilivyosajili watahiniwa, sawa na ongezeko la vituo 117 ikilinganishwa na ile ya mwaka 2011.


ISOME TAARIFA KAMILI YA MATOKEO HAYO YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA PILI, 2012 KAMA ILIVYOTOLEWA NA MHE, MULUGO


1.0UTANGULIZI
Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili ulifanyika nchini kote kuanzia tarehe 05/11/2012 na kumalizika tarehe 16/11/2012. Mwaka 2012 kulikuwa na jumla ya vituo 4,304 vilivyosajili watahiniwa, ikiwa ni ongezeko la vituo 117(2.79 %) ikilinganishwa na ile ya mwaka 2011.
2.0WATAHINIWA WALIOSAJILIWA, WALIOFANYA NA WASIOFANYA MTIHANI
2.1Idadi ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 430,327, kati yao wasichana walikuwa 205,476 na wavulana 224,851. Idadi hii ni upungufu wa watahiniwa 36,240 (7.76%) ikilinganishwa na mwaka 2011 ambapo walikuwa 466,567.
2.2Watahiniwa 386,271 sawa na asilimia 89.76 ya waliosajiliwa, walifanya mtihani wakiwemo wasichana 187,244 na wavulana 199,027.
2.3Watahiniwa 44,056 sawa na asilimia 10.24 hawakufanya mtihani, kati yao wasichana ni 18,231 na wavulana 25,825. Mwaka 2011 watahiniwa 47,527(10.19%) hawakufanya mtihani. Sababu za watahiniwa kutofanya mtihani ni pamoja na utoro, kuugua, kudaiwa ada, kufukuzwa shule, mimba na vifo.

3.0UFAULU WA WATAHINIWA
3.1Watahiniwa waliofaulu ni 249,325 (64.55 %) kati yao, wasichana ni 113,213 na wavulana 136,112. Kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 19.15 kutoka asilimia 45.40 mwaka 2011. Watahiniwa waliofaulu kwa kiwango cha A, B, na C walikuwa 127,981 (33.13%) na waliofaulu kwa kiwango cha D ni 121,344 (31.42%). Alama ya juu ya ufaulu ni 92%
3.2Wastani wa ufaulu kwa masomo ni 38%, wastani huu umepanda kwa asilimia 7 ukilinganishwa na mwaka 2011 ambapo ulikuwa 31%.
3.3Watahiniwa 136,923 (35.45 %) hawakufaulu mtihani, wakiwemo wasichana 74,020 na wavulana 62,903. Watahiniwa hawa watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013. Aidha, mwaka 2011 watahiniwa 228,759 (54.59%) hawakufaulu mtihani.
3.4Watahiniwa 23 matokeo yao yamefutwa kutokana na tuhuma za udanganyifu. Watahiniwa hawa wanatoka katika shule zifuatazo;
Na
Jina la Shule
Kanda
Idadi ya watahiniwa
1.
Kiyongwire
Mashariki
2
2.
Nyashishi
Ziwa
4
3.
Thaqaafar
Ziwa
3
4.
Paroma
Ziwa
2
5.
Murangi
Ziwa
1
6.
Bukene
Magharibi
7
7.
Kili
Magharibi
1
8.
Binza
Magharibi
1
9.
Kizumbi
Magharibi
1
10.
Kolandoto
Magharibi
1

Watahiniwa hawa nao watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013.

4.0UFAULU KWA SHULE
4.1Shule Zilizoshika Nafasi Kumi za Mwanzo
4.1.1Shule za Serikali
NA.
SHULE
KANDA
1.
MZUMBE
MASHARIKI
2.
TABORA WAVULANA
MAGHARIBI
3.
ILBORU
KASKAZINI MAGHARIBI
4.
KIBAHA
MASHARIKI
5.
IYUNGA
NYANDA ZA JUU
6.
MSALATO
KATI
7.
MALANGALI
NYANDA ZA JUU KUSINI
8.
IFUNDA UFUNDI
NYANDA ZA JUU KUSINI
9.
SAMORA MACHEL
NYANDA ZA JUU
10.
KILAKALA
MASHARIKI

4.1.2Shule Zisizo za Serikali
NA.
SHULE
KANDA
1.
KAIZIREGE
ZIWA MAGHARIBI
2.
MARIAN WAVULANA
MASHARIKI
3.
ST. FRANCIS
NYANDA ZA JUU
4.
DONBOSCO
NYANDA ZA JUU KUSINI
5.
BETHEL SABS
NYANDA ZA JUU KUSINI
6.
MARIAN WASICHANA
MASHARIKI
7.
DON BOSCO (MOSHI)
KASKAZINI MASHARIKI
8.
CANOSSA
DSM
9.
ST. JOSEPH ITERAMBOGO SEM.
ZIWA MAGHARIBI
10.
CARMEL
MASHARIKI

4.2Shule zilizoshika nafasi kumi za Mwisho
4.2.1Shule za Serikali

NA
SHULE
KANDA
1.
MIHAMBWE
KUSINI
2.
DINDUMA
KUSINI
3.
KIROMBA
KUSINI
4.
MARAMBO
KUSINI
5.
MBEMBALEO
KUSINI
6.
KINJUMBI
KUSINI
7.
LITIPU
KUSINI
8.
LUAGALA
KUSINI
9.
MIGURUWE
KUSINI
10.
NAPACHO
KUSINI

4.2.2Shule Zisizo za Serikali
NA.
SHULE
KANDA
1.
MFURU
MASHARIKI
2.
PWANI
MASHARIKI
3.
DORETA
KATI
4.
KIGURUNYEMBE
MASHARIKI
5.
RURUMA
KATI
6.
AT-TAAUN
MASHARIKI
7.
JABAL HIRA SEM
MASHARIKI
8.
MKONO WA MARA
MASHARIKI
9.
KILEPILE
NYANDA KUSINI
10.
KIUMA
NYANDA KUSINI



5.0UFAULU WA WANAFUNZI
Wanafunzi Walioshika Nafasi Kumi za Mwanzo
Na
JINA
JINSI
SHULE
1.
MAGRETH KAKOKO
KE
ST FRANCIS
2.
QUEEN MASIKO
KE
ST FRANCIS
3.
LUKUNDO MANASE
ME
KAIZIREGE
4.
FRANK J NYANTARILA
ME
KAIZIREGE
5.
GRACE MSOVELLA
KE
ST FRANCIS
6.
HARIETH MAKIRIYE
KE
ST FRANCIS
7.
ROBINNANCY MTITU
KE
ST FRANCIS
8.
HUMRATH LUSHEKE
KE
ST FRANCIS
9.
MUKHSIN HAMZA
ME
KAIZIREGE
10.
ANASTAZIA KABELINDE
KE
KAIZIREGE









6.0HITIMISHO
Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili mwaka 2012, yanaonesha kuwa kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka asilimia 45.40 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 64.55 mwaka 2012. Aidha, watahiniwa 249,325 wataendelea na masomo ya kidato cha tatu mwaka 2013. Napenda kuwapongeza wanafunzi wote waliofaulu kuendelea na masomo na kuwataka kuendelea na bidii katika kujifunza.
Kwa upande mwingine, watahiniwa 136,946 ambao wameshindwa kupata wastani wa ufaulu wa alama 30 na wale waliofutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013. Ni vema ikaeleweka kuwa kukariri kidato si adhabu bali ni kutoa fursa nyingine kwa mwanafunzi kuweza kupata maarifa, stadi na ujuzi wa elimu ya sekondari kidato cha kwanza na cha pili kwa kiwango kizuri. Hivyo ni matumaini yangu kuwa wanafunzi hawa watafanya bidii katika kujifunza na kuzingatia masomo ili waweze kufaulu, pia walimu kuwasaidia Wanafunzi hao waweze kufanya vizuri.
Serikali kwa upande wake itaimarisha usimamizi wa elimu katika ngazi ya shule na kuziwezesha shule kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ikiwa ni pamoja na walimu kubadili mikakati ya ufundishaji na ujifunzaji na wazazi kufuatilia maendeleo ya wanafunzi.
Vilevile, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) itaendelea na jitihada zake za kuimarisha na kuboresha mazingira ya utoaji elimu bora kwa kujenga maabara za sayansi, kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu, kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kuimarisha usimamizi wa shule. Aidha, wizara itaendelea kutoa walimu kwa awamu kila mwaka ili kukabiliana na upungufu uliopo.
Mhe. Philipo Mulugo (Mb)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
11/01/2013
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top