“Hiki ni kiwango cha juu kabisa kwa nchi kuweza kukopa kutoka kwenye masoko
ya kimataifa, deni limeongezeka kwa dola 456.1 milioni katika kipindi cha mwaka
mmoja tu tangu Oktoba 2011,” alisema Mwakagenda.Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ya Tanzania Coalition on
Debt and Develompent (TCDD), Hebron Mwakagenda akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu kuongezeka kwa deni la taifa kufikia
kiasi cha Sh22 trilioni hadi Oktoba mwaka jana. Kulia ni Ofisa Mipango, Boniface
Komba. Picha na Fidelis Felix.
TAASISI isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na
masuala ya Madeni ya Taifa na Maendeleo (TCDD), imesema kitendo cha Serikali
kukopa fedha kwa ajili ya matumizi yasiyo na umuhimu pamoja na kuwalipa
watumishi wake mishahara, kimesababisha taifa kuwa na deni la Sh22
trilioni.
Imesema hali hiyo ni hatari hasa ikizingatiwa kuwa
miaka kadhaa iliyopita, Tanzania kupitia Mpango wa Nchi Maskini zenye Madeni
Makubwa (HIPC), ilifutiwa kiasi kikubwa cha madeni , lakini sasa imeanza kukopa
tena.
Taasisi hiyo pia imesema kitendo hicho kimechangia
kuporomoka kwa uchumi wa taifa kwa sababu mikopo hiyo ina riba
kubwa.
Imeeleza kuwa Serikali inakopa fedha hizo Benki Kuu (BoT), Benki za Biashara, Kampuni za Bima na Mashirika ya Hifadhi za Jamii, Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) na Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF).
Imeeleza kuwa Serikali inakopa fedha hizo Benki Kuu (BoT), Benki za Biashara, Kampuni za Bima na Mashirika ya Hifadhi za Jamii, Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo Afrika (ADB) na Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo ambayo kazi yake kubwa ni kuishauri
Serikali katika suala zima la deni la taifa na maendeleo, Hebron Mwakagenda,
alisema hadi kufikia Oktoba mwaka jana, deni la nje lilikuwa Sh15.9
trilioni.
“Hiki ni kiwango cha juu kabisa kwa nchi kuweza kukopa
kutoka kwenye masoko ya kimataifa, deni limeongezeka kwa dola 456.1 milioni
katika kipindi cha mwaka mmoja tu tangu Oktoba 2011,” alisema
Mwakagenda.
Alisema taarifa za Benki Kuu ya Tanzania zinaonyesha
kuwa deni la ndani limefikia Sh5.1 trilioni hadi kufikia Oktoba mwaka jana na
kwamba kiasi hicho ni sawa na ongezeko la Sh513 bilioni tangu mwaka
2011.
“Deni la ndani linakua kwa kasi kubwa inayotokana na
Serikali kuanza kukopa kwenye benki za biashara ambazo zinatoza riba kubwa. Hii
ni hatari kwa uchumi wa nchi,” alisema Mwakagenda.
Alisema zipo fedha zinazotumika kujenga barabara,
madaraja, majengo mbalimbali ya shule na vyuo, lakini kinachotakiwa ni Serikali
kufikiri mara mbili kabla ya kuamua kukopa na kuzitumia fedha hizo za
mkopo.Katika mapendekezo yao, Mwakagenda alisema wameitaka Serikali kuwa na
nidhamu katika kukopa kwa kuwa deni hilo limevuka kiwango cha
kimataifa.
“Pia umefikia wakati kwa Serikali kutokopa mpaka ipate
ridhaa ya Bunge kwa kuwa mikopo mingine haina faida kwa taifa zaidi ya kuwaumiza
wananchi,” alisema.
Alisema kuwa hadi sasa hakuna juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha kuwa inapata mikopo yenye riba nafuu.
Alisema kuwa hadi sasa hakuna juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha kuwa inapata mikopo yenye riba nafuu.
Alisema kitendo cha Serikali kuendelea kukopa
kutaifanya nchi kutoaminika tena na hivyo kutokopesheka iwapo kutaibuka mahitaji
ya lazima.
“Pia wawekezaji wanaweza kupunguza imani na mazingira
ya kiuchumi ya Tanzania na hivyo kutokuja kuwekeza, nchi itashindwa kulipa
madeni, thamani ya shilingi itashuka,” alisema
Mwakagenda.
Alisema Serikali inatakiwa kujifunza kwa nchi za
Hispania, Ugiriki na Ireland ambazo zimekubwa na matatizo ya kiuchumi kutokana
na kuwa na madeni makubwa.
“Tunaelezwa kwamba deni la taifa ni endelevu na bado nchi inakopesheka, sijui wanatumia takwimu za wapi,” alisema.
“Tunaelezwa kwamba deni la taifa ni endelevu na bado nchi inakopesheka, sijui wanatumia takwimu za wapi,” alisema.
Post a Comment