Mbunge wa Jiji la Arusha Godbless Lema (pichani) amelipongeza jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kuweza kudhibiti vitendo vya uhalifu wakati wa kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka na kulitaka jeshi hilo kutoa ushirikiano kwa wananchi sanjari na kuacha kazi za siasa na badala yake kazi ya siasa kuziachia CCM na Chadema.
Lema ameyasema hayo wakati alipofika kwenye ofisi yake kwa mara ya kwanza tangu mahakama kuu ilipotengua matokeo ya ubunge wake hadi mahakama ya rufaa ilipomrudishia ubunge huo mwisho mwaka jana.
Post a Comment