![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCbm7y9p1l9zj3cQdjXQnL64WpUm2y6dxheqVzxvXJl45iHQ8dGjihv6Q2v-aIRJ1WjK24IIlMh5LOo2J5O9qFELnWVgcibIhS_pqv8Kv0oSjVjgXKS-KYZICX44j4_xmUPyXYkQOvj9M/s640/ig2.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjUmmQ_FiHD2GA4cezBg1-5CrArdiVG1U4xa26GAS3_c74qvtVPDyR48ePIzW-K0unk2p3JngpDyfOzwTCYMmC3HA41o_aRAA640VM0uwE-NV4daH8Vgn_uXwxd0J47D_r2-eZ8MKHKBeE/s640/mbu2.jpg)
Wananchi wakivuka kwa taabu sehemu ambako daraja la bonde la Mbutu
wilayani Igunga linajengwa na kuondoa kabisa tatizo hilo mwaka huu
ambapo ujenzi huo unaofanywa na muungano wa makandarasi wa Tanzania
unatarajiwa kukamilika. Mpaka sasa asilimia 45 ya ujenzi wa daraja hili
lenye thamani ya sh bilioni 11.28 umekamilika na inakadiriwa kuwa litakuwa
tayari ifikapo Novemba mwaka huu.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhoymK_2jBb76wjZNNhI_zsCVTXGbFTTK0kxZxIWhQbfXFUHBDJ3wvuWFogidr-9rNzBNzv6p1V8cxKgiI0P3PWQg7l3E_4Cbq3du7N2n6pvMRbCEtrFWz1IO1SqH_7lJURSA6hURYtlIs/s640/ig10.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjBgLtxauhxKGmWvUaQBgq87cXPvICnxIRAn4ZWQ__MZNE_6AXIzIOPI2BDccJHUZA03Tjz4_y3pidIVjEhX5wB7TmvztEd4gwtfy92cguWpwGcrOMRAWXQwfqTBdp6hdPI1KevebykXVs/s640/ig7.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZ4lYlJbuutNncu2wMRn4g4e_uk34GUi-oWski5_3W4GRiaxix0LK5TgSIfWnzOAGnq2Xd9RqVIBZyds64YJwhxz02N1uULJi-qkDeGazZXF6rDcWmSJnZHD_q8V390LV3SXdhvPWYC20/s640/mbu18.jpg)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi mashimo yatayosimikwa nguzo za daraja hilo yanavyochimbwa
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj97-eqAjSdn1VgwQPbaQI7R3vlCuz1c37BTsdAFFobeS8XT0s_1lfnwc53M7R11daKobu3lz8z25df37tn4GLRxaoyN-hFUkgcmFmHfC6_KFWRwKvO4liP4yCYD7SrJVbforrwayFlUTM/s640/ig6%25281%2529.jpg)
Rais Jakaya Mrisho Kikwetea akipata maelezo ya Uzinduzi mradi wa Chujio
la maji safi kwa mji wa Igunga sehemu za Bulenya ambapo wakazi asilimia
70 wa mji huo watapata maji safi
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjUFUU_ousUKegmpU6oryw_GOGb9pKC6JnthPTUArrd1drgjMvvpIA0a3wJocLjpu_8cJvHLo6HJEKDI94cR5D9cnrXhsuARO9Re_6MhkU48NZdakZwctQsGUgWX7tduRmlwuFclNfWJGM/s640/mbu19.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3KnQKUXvk-5GFfTzBXaJGFuWC5hQupxrVMG-iZcDUICTQdZhkArrWMtNQU2wNIMuRMqUCbVEeYk5Gb5MzcXnhEGdbforqKj-qrQ1YwnSbYorYRBhdwFSMe9WuvvkGkRmpSLV8C-I9vjQ/s640/ig9.jpg)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mawaziri, wabunge na maofisa
waandamizi wa wizara na wakala wa ujenzi (TANRODS) pamoja na viongozi wa
bodi ya wakandarasi akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa daraja hilo
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhoymK_2jBb76wjZNNhI_zsCVTXGbFTTK0kxZxIWhQbfXFUHBDJ3wvuWFogidr-9rNzBNzv6p1V8cxKgiI0P3PWQg7l3E_4Cbq3du7N2n6pvMRbCEtrFWz1IO1SqH_7lJURSA6hURYtlIs/s640/ig10.jpg)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mawaziri, wabunge na maofisa
waandamizi wa wizara na wakala wa ujenzi (TANRODS) pamoja na viongozi wa
bodi ya wakandarasi akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa daraja hilo
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiX04_elpeO37oICA05THTPA5Wd1ZjtTT0JPidyY2e0wq7icC75psL4Jn81QWT0GcKTiHvr2OUYyV7OhSaurotlCXdtxsUfW0hdRp0zLOFeoCv_JaBJH2ih80_q-fsziAq2TJdIe0bmgEs/s640/mbu20.jpg)
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakipozi na umoja wa
wakandarasi wazalendo kutoka makampuni mbalimbali waliopewa kandarasi ya
kujenga daraja hilo.
-----
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiIzSbiR8zi8oR8XTqK-CA-RhqfDYcnKVnDOOTWnzX7KpdjRBVXiFEWEajSdLVpTu2BpnmoJqG1y7FzUx61QMQ5cuwhNDLGw4sNSYS28gL9dfJ_tni-vhh-SQnwk6f1-dHnrkph8OZD5xnf/s1600/251px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png)
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Serikali
yake inakaribia kukamilisha ujenzi wa madaraja yote
10 yaliyoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na ambayo
yanagharimu mabilioni ya fedha.
Rais Kikwete amesema kuwa kati ya madaraja hayo ambayo
thamani yake inakaribia sh. bilioni 415, madaraja mawili tayari ujenzi
wake umekamilika. Madaraja hayo ni lile la Ruhekei lililoko Wilaya ya
Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma na Daraja la Mwatisi katika Mkoa wa Morogoro.
Rais Kikwete amesema kuwa madaraja mengine saba yanaendelea
kujengwa, ikiwa ni pamoja na Daraja la Kigamboni, Mkoa wa Dar
es Salaam linalogharimu sh bilioni 214.6, Daraja la Kikwete katika Mto
Malagarasi, Mkoa wa Kigoma unaogharimu sh bilioni 90.185, Daraja la
Kilombero, Mkoa wa Morogoro linalogharimu sh bilioni 53.214 na Daraja
la Rusumo, Mkoa wa Kagera linalogharimu sh bilioni 31.7.
Madaraja mengine yanayoendelea kujengwa ni Daraja
la Sibiti, Singida, linalogharimu sh bilioni 17.5, Daraja la Nangoo,
Mkoa wa Mtwara linalogharimu sh bilioni 4.29 na Daraja la Maligisu,
Mwanza, linalogharimu sh bilioni 2.51.
Amesema Rais Kikwete: “Madaraja niliyotaja ujenzi
wake ukikamilika, tutakuwa tumetimiza ahadi yetu ya kujenga madaraja
yote yaliyotajwa katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 isipokuwa Daraja
la Ruhuhu ambalo maandalizi yake ya ujenzi yanaendelea.”
Rais Kikwete alikuwa anazungumza wakati anaweka jiwe
la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Mbutu, Wilaya ya Igunga,
Mkoa wa Tabora katika sherehe ya kufanya iliyofanyika Jumatatu,
Januari 7, 2013.
Rais Kikwete amesema kuwa baadhi ya madaraja yanayojengwa
sasa na Serikali yalipangwa kujengwa katika Mpango wa Pili wa Taifa
wa Maendeleo mwaka 1968 lakini kwa bahati mabaya hayakuweza kujengwa.
Madaraja hayo ni Daraja la Kigamboni, Daraja la Kirumi kwenye Mto Mara,
Daraja la Rufiji, Daraja la Kilombero, Mkoa wa Morogoro na Daraja la
Kikwete kwenye Mto Malagarasi.
Awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi yetu ilijenga
Daraja la Kirumi kwenye Mto Mara, Awamu na pili ikafanya maandalizi
na Awamu ya tatu ikajenga Daraja la Rufiji na Awamu ya sasa inajega
madaraja matatu yaliyobakia – Kilombero, Kigamboni na Kikwete.”
Daraja la Mbutu lina urefu wa kilomita tatu, na linajengwa
katika Bonde la Mbutu na litaunganisha mikoa ya Tabora, Singida, Simiyu
na Shinyanga.
Daraja hilo litakuwa na daraja moja kubwa la mita
60 na madaraja mengine madogo saba na hivyo kufanya urefu wa daraja
lote kuwa na mita 165. Mpaka sasa asilimia 45 ya ujenzi wa daraja hili
lenye thamani ya sh bilioni 11.28 umekamilika na inakadiriwa kuwa litakuwa
tayari ifikapo Novemba mwaka huu.
Mwisho.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Post a Comment