Kama
inavyojulikana kuwa mwanamuziki Jay Z na mkewe Beyonce wanaishi maisha
ya juu yenye hadhi ya kifalme vivyo hivyo binti yao Blue Ivy Carter
anastahili huduma zenye kiwango hicho hicho.
Kwanza
ikumbukwe kuwa binti huyo alizaliwa katika chumba maalum katika
hospitali ya Lenox Hill ambacho sasa kimebatizwa jina la ‘Beyonce Room’.
Mwanamuziki
huyo ameamua kukodisha shule ya nasari kwa dola milioni 1 za Marekani
katika eneo maarufu la Barclays Center huko Brooklyn, hivyo kuhakikisha
Blue anapata elimu ya awali katika mfumo wa kifahari.
Jay
Z anayejulikana kwa kupenda kutizama mchezo wa mpira wa kikapu, hilo
ndilo eneo lake ambalo ni makazi ya timu ya Brooklyn Nets, na katika
sakafu ya ardhini mwanawe atakuwa akijipatia elimu ya awali kwa
kujinafasi.
Post a Comment