|
Jeshi la Polisi linaonekana kufanya
kazi zaidi kwa mazoea kuliko kuzingatia mafunzo wanayopewa, pichani ni askari
polisi aliyejeruhiwa na wenzake baada ya kupigwa marungu kwa kutomjua kama
nayeye ni askari hadi alipopiga kelele ‘mtaniua mimi mwenzenu’ ndipo
wakamuachia.
Kilichofuata baada ya askari huyo
kuachiliwa na wenzake alimalizia hasira zake zote kwa wanafunzi hao kwa
kutembeza kipigo (mkong’oto) mkali kwa wanafunzi Chuo Cha IFM waliojaribu kutaka
kulazimisha jeshi la polisi kufanya mkutano mbele ya kituo cha Polisi Kigamboni
badala ya kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava Kigamboni bila kujali kuwa
wanafunzi hao walikuwa wakikabiliana na moshi nzito wa mabomu ya machozi lakini
pia walisha kuwa chini ya ulinzi mkali na hakukuwa na sababu yeyote ya kuwapiga
hivyo.
Mbali na askari huyo kulikuwepo na
askari wengine wawili akiwemo mmoja wakike naopia waliambulia kipigo hiko.
Fuatilia picha za Askari huyo na matukio aliyofanya
.
|
|
Picha hii inakuonesha kwa
karibu namna rungu lilivyompasua Askari huyu, hapa utapata picha kama huyu
askari aliyepigwa kidogo tu baadaye akaachiwa ameumia hivi je wale waliopata
mkong'oto wapo kwenye hali gani. |
|
Hapa anazuia damu sehemu
aliyopigwa isindelee kuvuja kwa kutumia
kitambaa. |
|
Baada ya kupata nafuu
anakuja kumalizia hasira zake kwa wanafunzi kwa kumkamata mmoja na kumpa kipigo
cha nguvu hadi askari wenzake walivyopiga kelele ndipo alimwachilia mwanafunzi
huyo. |
|
Hakuishia hapo aliwafuata
pale walipoamrishwa kukaa akawa anamchomoa anaemtaka na kumpa kipigovile
alivyojiskia ili amalizie hasira zake. |
|
Kumbuka kipigo hicho kinafanyika mbele ya kituo cha polisi
huku kukiwa na ulinzi mkali umeimarishwa. |
|
Alichagua kama maembe au
mpira na kuchezea alivyotaka! |
BAADA ya
wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda wa
kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao
hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa,
waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka
mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi
wengi wao walielekea huko.
Mara baada
ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa maratatu waondoke waende kwenye mkutano
na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo ndipo mabomu yakaanza kupigwa. Kwenye
mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa na kuumia wengine walipoteza
fahamu.
Hata hivyo
walioshikiliwa wote waliachiwa na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao
uliazimia mambo kadhaa ya utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye
eneo hilo. Kamanda Kova aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua
walizochukuwa siku ya tarehe 30 mwezi huu.
Post a Comment