*ADAI SERIKALI IMEAGIZA MTAMBO WA KUHUJUMU MAWASILIANO YA WAPINZANI
* YADAIWA "UFYATUKAJI" NDIYO NJIA YAKE YA KIPEKEE YA KUONGEZA UMMARUFU WA KISIASA
.
DK SLAA.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa amebaini kuwapo mpango wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuingiza mtambo wa kuingilia mawasiliano ya wapinzani kwa ajili ya kuhujumu uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Dk. Slaa ambaye ni mara yake ya pili kutoa tuhuma za CCM kuingiza mtambo wa kuingilia mawasiliano ya CHADEMA, alisema tayari ameshapata e-mail yenye kuonyesha thamani ya mtambo huo na kwamba utagharimu dola 850,000 za Marekani, karibu sawa na sh bil. 1.3.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua kongamano la vijana wa vyuo vikuu wa CHADEMA (Chaso), jijini Dar es Salaam, lililokuwa na lengo la kujitathmini na kupanga mikakati ya kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015 pamoja na kuwaapisha viongozi wapya wa shirikisho hilo.
Alisema tayari ameshaandika barua kwa mamlaka husika kuwajulisha hilo, lakini hadi sasa hawajajibu.
“Tuna ‘details’ na nyaraka nyingi zinazoonesha namna mtambo utakavyotumika kwa ajili ya kuwahujumu wapinzani na kwa kuwa tumeshaandika barua kwa mamlaka husika na hawajatujibu, kwa sasa sitaenda kwa undani zaidi juu ya hili. Subirini siku ifike nitaweka kila kitu hadharani,” alisema Dk. Slaa.


Post a Comment