Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

LORI LA TEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI


 Roli hilo likiondolewa eneo hilo la mzunguko wa magari eneo la Msamvu Morogoro
                               Wananchi wakishuhudia tukio hilo




 Kontena lililojaa mzigo wa shehena ya ngano iliyokuwa akisafirisha na roli hiyo kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kigoma  lilinusulika kuungua na moto huo kama linavyoonekana pichani
 Mmoja wa wafanyazi wa wakala wa barabara mkoa wa Morogoro'TANROARD' akifagia mabaki wa roli hilo.
 Roli hiyo  lenye namba za usajiri T 281 BHG baada ya moto kuzimwa lilibaki vyuma chakavu 'skrepa'
 Chanzo cha moto huo inadaiwa ni roli hilo kuangukia eneo hilo la mzunguko wa barabara na betri ya gari hilo ambalo mara nyingi huwekwa kwenye chesesi upande wa wa kushoto jirani na tenki la mafuta,liligonga  eneo hili na kupasuka ambapo hali hiyo ilisababisha  shoti kali iliyozua moto huo.



audifacejackson.blogspot.com.
ROLI la mizigo lenye namba za usajiri T 281 BHG ambalo lilikuwa likisafirisha shehena ya ngano kutoka jijini Da r es salaam kueleka mkoani Kigoma.leo asubuhi limepinduka na kuteketea kwa moto ndani ya  mzunguko wa barabara eneo la Msamvu mkoani Morogoro.audifacejackson.blogspot.com..
Akizungumza na Mtandao huu eneo la tukio askali mmoja wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro,ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa yeye sio msemaji wa jeshi hilo,alidai kwamba chanzo cha moto huo ni roli hilo kuzunguka kwa kasi mzunguko huo na kupinduka kisha betri ya gari hilo kupasuka na kusababisha moto huo.audifacejackson.blogspot.com." kama sio juhudi za wafanyazi wa kikosi cha zima moto mazara ya moto huu yangekuwa makubwa kwani tukio hili limetokea jirani na kituo cha mafuta kilichopo jirani na mzunguko huu wa barabara,kwa bahari hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha kwenye janga hili"alisema Trafik huyo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top