Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AFUNGUA SKULI YA MBUYU TENDE ZANZIBAR


 

 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna mara alipowasili katika Kijiji cha Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini “A”kwa ajili ya kufungua Skuli ya Primary yenye madarasa Manne,ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikata Utepe kuashiria kufungua Skuli yenye madarasa manne katika Kijiji cha Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini “A”,ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akipanda Mche wa Mnazi baada ya kuupanda katika eneo la Skuli ya Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini “A”,Baada ya Kuifungua Skuli hiyo ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Wanafunzi wa Skuli ya Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini “A”,wakifurahia Baada ya kufunguliwa kwa Skuli yao ikiwa ni Shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad amewataka Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wa Skuli ya Mbuyu Tende kujenga Mashirikiano na Walimu ili kuweza kuwapatia haki na fursa sawa wanafunzi wa kike na wakiume Skulini hapo.
Hayo ameyasema leo huko Skuli ya Msingi Mbuyu Tende Wilaya Kaskazini “A” Unguja wakati wa ufunguzi wa skuli hiyo ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Maalim Seif amewataka Wazazi wasikubali kuwaozesha watoto wa kike waume mapema kwani hali hiyo ndiyo inayochangia ukosefu wa Walimu wa kike wazawa katika Vijiji vingi.
Aidha alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kuwapatia wananchi wake haki ya elimu bila ya malipo ili kuondosha adui ujinga na kuwaletea maendeleo.
“Elimu ni msingi wa maisha kwa vijana na ndio inayoleta maendeleo na mwangaza hasa wakati wa sasa na ujinga ni kiza katika maisha ya leo,”alisisitiza Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Alisema kuwa wanafunzi wakipata msingi mzuri wa elimu wataweza kupambana na mazingira ya sasa ya sayansi na teknolojia kwa kwa ufanisi mkubwa.
“Tusitazamie vijana kupata maisha mazuri bila ya elimu hasa katika zama hizo za sayansi na tecnologĂ­a kwani elimu ndio kila kitu’’alisema Makamo wa Kwanza .
Maalim Seif aliitaka Idara ya Mitaala kuandaa mbinu bora za ufundishaji wa mafunzo ya amali ili wanafunzi wakimaliza masomo yao waweze kujiajiri wenyewe na kuweza kuondosha mzigo kwa Serikali.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna alisisitiza wananchi wa kijiji hicho kuchukua juhudi ya kuwasimamia watoto wao hasa wa kike kupata elimu kwani wanauwezo wa kufanya vizuri zaidi katika masomo.
Aidha katika uzinduzi huo zaidi ya shilingi milioni 11 zilichangwa kwa ajili ya maendeleo ya skuli hiyo ambapo Makamu wa Kwanza wa Rais alichangia milioni tano na Waziri Shamhuna milioni tatu.
Ujenzi wa Skuli ya Mbuyu Tende umegharimu jumla ya shiling Milioni 44 kwa ajili ya kujengea jengo lenye madarasa manne pamoja na kununua madawati kwa Skuli hiyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top