Kamanda wa polisi mkoa wa
Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
pambano la ngumi la kutetea ubingwa Afrika mashariki na kati kati ya bondia
Mtanzania Thomas Mashali na Bernad Mackoliech wa Kenya Jumamosi katika Ukumbi wa
Friends Corner Manzese.
Akizungumza na waandishi wa
habari mratibu wa pambano hilo Aisha Mbegu alisema wameamua kumualika kamanda
Kenyela ili kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kutoa Elimu ya Ulinzi shirikishi
na kwa kutambua mchango wa jeshi la polisi kudumisha amani katika
michezo.
“ Jeshi la polisi ni wadau
wetu wakubwa katika michezo hasa ngumi na mchango wao umekuwa ukionekana kwani
sasa hakuna vurugu zinazojitokeza katika mapambano yeyote ya ngumi yanayofanyika
tofauti na Miaka ya Nyuma ambapo Ngumi ilikuwa Watoto hawawezi kwenda
kuangalia,”alisema Aisha.
Aisha alisema katika
pambano la awali ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa Friend corner hakukuwa na
vurugu na idadi ya watoto na wanawake kuangalia ngumi imekuwa ikiongezeka siku
hadi siku na nhivyo kutoa hamasa kwa wazazi na watoto kupenda mchezo
huo.
Mbali na Kenyela Mbunge wa
Kinondoni Iddi Azan na Mbunge wa ubungo John Mnyika wamealikwa ili kushuhudia
vipaji vya vijana
wa kinondoni katika Ngumi.
Bondia Mackoliech
anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari leo (Alhamisi) katika Uwanja wa
Karume na Ijumaa wanatarajiwa kupima Uzito saa Nne asubuhi katika Ukumbi wa
Friends Corner Manzese .
Post a Comment